Nini Tunafadhili

Kupitia utoaji wa Ruzuku, Foundation inafadhili miradi inayotekelezwa kwa lengo kuwajengea uwezo wananchi hasa masikini na walio pembezoni na makundi mengine yaliyo katika hatari ya kuathirika zaidi ili makundi hayo yaweze kushiriki katika mipango ya maendeleo na kupunguza umasikini.
Maeneo makuu yanayofadhiliwa na Foundation ni:


(i)    Ushiriki katika utungaji wa sera na ufuatiliaji wake :
Foundation itawezesha miradi yenye lengo la Kuwezesha wananchi kushiriki na  kufuatilia utekelezaji wa sera katika kuimarisha utoaji wa huduma. Kuwezesha sauti za wananchi kusikika kiikamilifu katika utungaji wa sera ili waweze kuboresha maisha yao.
Mifano ya shughuli zilizopo katika utungaji wa sera na utekelezaji wake ni pamoja na:
•    Ufuatiliaji wa miradi shirikishi ya kupunguza umasikini, ambayo inalinganisha na kutofautisha habari juu ya umasikini na kuzisambaza eneo pana.
•    Kupanga mipango ndai ya jamii juu ya jinsi mabadiliko ya sera Fulani yanavyoathiri maisha yao na jinsi watakavyoitikia.
•    Ushiriki wa jamii katika kupanga vipaumbele kwa ajili ya sera za kitaifa
•    Kuinua ufahamu wa umma juu ya masuala ya sera.
 
(ii) Kuimarisha Utawala bora na haki za kiraia
Foundation husaidia asasi zote ambazo zinaamsha uelewa wa watu kuhusu haki zao na majukumu ya Serikali, kuimarisha ushirikiano kati ya asasi zinazofanya kazi katika masuala ya haki za binadamu katika ngazi za chini na kitaifa na kuongeza upatikanaji wa haki kwa wananchi wote wa Tanzania.
 Foundation itatoa ruzuku kwa miradi ambayo itawezehsa taasisi za serikali, umma na binafsi kuwa wazi zaidi, kuwajibika na kuheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu. Mahususi, Foundation itafadhili miradi ambayo itahakikisha wananchi wanafahamu haki na wajibu wao, waweze kudai uwajibikaji kutoka katika rasimimali za umma na hivyo miradi itakuwa na athari chanya.
Mifano ya shughili chini ya Utawala Bora na Uwajibikaji ni pamoja na:
•    Mikutano ya hadhara juu ya sera za Taifa\Vipindi vya redio juu ya masuala ya utawala bora kama vile Rushwa
•    Michezo ya kuigiza shirikishi inayoamsha uelewa wa haki za binadamu
•    Mafunzo ya viongozi wa Asasi za Kiraia na serikali za mitaa juu ya mabadiliko katika wajibu na majukumu chini ya maboresho ya serikali za mitaa.
 
(iii) Kuimarishwa kwa Uwezo wa Asasi za Kiraia
Foundation inasaidia Asasi za Kiraia zinakuwa nguzo imara ya kuleta mabadiliko, kufanikisha malengo yaliyokusudiwa na inatekeleza wajibu wake wa utetezi kwa vipaumbele vya maendeleo. Tunapenda kuona sekta ya asasi za kiraia yenye ari, ubunifu, inayotimiza majukumu yake endelevu na inayowajibika ambayo inachangia kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kudumu katika maendeleo nchini Tanzania.
Mifano ya shughuli zilizopo chini ya Uimarishaji wa Asasi za Kiraia ni pamoja na:
•    Kuimarisha mitandao
•    Kujenga uwezo
•    Kuunda na kusaidia mitandao ya Wilaya
•    Mafunzo ya stadi katika uchambuzi wa sera na utetezi kwa ajili ya wafanyakazi. In all the

Katika maeneo yote hapo juu, kuwahusisha masikini na makundi maalumu ni muhimu. Ubunifu unahimizwa sana. The Foundation inapendelea miradi ambayo inatumia mbinu za kuwafikia watu wengi zaidi, mfano kutumia vyombo vya habari kuhakikisha idadi kubwa ya wananchi inalengwa na miradi inayofadhiliwa..