Maeneo ambayo hayatafadhiliwa na Foundation


Foundation inaweza kutoa ruzuku kwa asasi ambazo zimeanzishwa si kwa nia ya kupata faida au kwa ufupi hazizalishi ka nia ya kupata faida. Hata kama mradi ulioombea si wa faida, hutakuwa na nafasi ya kupata ruzuku kama katiba haionyeshi wzi kwamba asasi yako imeanzishwa kwa ajli ya huduma na wala si kutengeneza faida. Kama unadhani kwamba asasi yako itakabiliwa na sharti kama hili tafadhali pata ushauri kutoka kwentu kabla hujaandika maombi ya ruzuku.


Foundation haitatoa ruzuku kwa: Fedha za kutunisha mfuko na masaada wa masomo au utaalamu, mradi au shughuli ambazo zipo nje ya Tanzania, mradi au shughuli ambazo zimemalizika; mradi ambayo unataoa ruzuku kwa taasisi nyingine; bakshishi kwa ajili ya wafanyakazi wa asasi na mradi inayozalisha faida.


Pia maombi ya ruzuku kwa wataalamu wa kuchangisha fedha au washauri ambao wanajitegemeza kwa niaba ya asasi;mtu binafi, vyama vya siasa, mradi ambao unapendelea dini Fulani, sekta binasi (labda iwe chama kisichotengeneza faida, asasi ambazo zina madeni makubwa na utaojai wa hduuma za jamii.


ZINGATIA: Taasisi zote ambazo huendesha shughuli za utoaji mikopo kwa vyama vya kuweka na kukopa, taasisi za kifedha zinazotoa mikopo hata ile midogo au wale ambao biashara ya fedha ndio mhimili wao mkubwa wanatakiwa kuwasilisha mchakato ambaoa umeweka wazi na wenye ushawishi mkubwa kuhusu mradi wao kama watataka kushughulikia masuala nje na utaratibu wao wa kawaida wa biashara ya fedha. Foundation haitatoa fedha kwa ajli ya kukopesha watu binafsi au makundi.