Nani Anaweza Kuomba


JE NANI ANAWEZA KUOMBA RUZUKU?

Tunakaribisha maombi kutoka kila sehemu ya nchi. Asasi yako inaweza ikatuma maombi ya ruzuku iwapo ninyi ni:

  • Asasi isiyo ya kiserikali (NGO)
  • Jumuia ya Kijamii (CBO)
  • Chama cha Kitaalamu
  • Chama cha Wafanyakazi
  • Shirika la Habari
  • Shirika la kidini
  • Ushirika.

Na kama:

Asasi yako imesajiliwa Tanzania Bara na/au Zanzibar Asasi yako imeanzishwa kwa madhumuni ya hisani (si kuzalisha faida Una katiba au sheria ndogondogo halali zinazotambulika zinazoyaeleza Madhumuni ya asasi yako na jinsi unavyoiendesha Asasi yako ina akaunti ya benki inayoendeshwa na watia saini zaidi ya mmoja Walau mwaka mmoja umekwisha tangu asasi yako ilipoanzishwa na kuanza kazi.

MATAWI YA ASASI KUBWA ZAIDI

Asasi ambayo ni tawi la asasi kubwa zaidi (ya kitaifa au kimataifa) inaweza kutuma maombi kama tu inathibitisha inafanya kazi zake bila ya kutegemea makao makuu.

UBIA AU MUUNGANO WA ASASI

Foundation inashauri na kutia moyo asasi kufanya kazi pamoja kushughulikia matatizo yanayofanana. Kama asasi mbili au zaidi zinazojitegemea zikituma maombi ya ruzuku kwa ajili ya kufanya kazi pamoja, tunawachukulia kama wabia au kikundi cha asasi mbili au zaidi.

ASASI ZA KIMATAIFA

Iwapo asasi yenu ni ya kimataifa ikiomba ruzuku kutoka Foundation, mnapaswa mkumbuke kwamba lengo la msingi la Foundation ni juu ya jumuia za kiraia za Tanzania, na mtatakiwa kuonyesha uhusiano mkubwa na uelewa wenu juu ya asasi za Tanzania.

MICHANGO KWA PROGRAMU ZA WAFADHILI WENGI (UFADHILI WA SEHEMU)

Foundation iko tayari kutoa sehemu ya fedha kwa mradi mkubwa ambao pia unafadhiliwa na wafadhili wengine. Unapaswa uonyeshe wazi jinsi na sehemu gani za mradi ambazo Foundation inaombwa izitolee fedha.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Ruzuku