Foundation for Civil Society ni nini?


Foundition for Civil Society (Foundation) ni asasi huru iliyoanzishwa Tanzania kama Kampuni isiyozalisha faida, inayofadhiliwa na kikundi cha wabia wa maendeleo Tanzania wenye mawazo yanayofanana, na inayoongozwa na Bodi iliyo huru.

DIRA

Kuwa mfano endelevu wa ubora ambao unachangia katika kujenga jamii ya makundi ya kiraia yenye ari na ubunifu, yatakayowawezesha wananchi kushiriki katika michakato ya kidemokrasia, kuendeleza haki za binadamu na kuchangia katika kupunguza umasikini na kuinua ubora wa maisha ya Watanzania wote.

Lengo: Kutoa ruzuku na kujengea uwezo asasi za kiraia ili ziwezeshe wananchi, ikiwa ni pamoja na makundi yaliyopembezoni kiuchumi na yale yenye uwezekano wa kuathiriwa zaidi na umasikini (vunerable groups) ili:

» Kupata taarifa na kuelewa haki zao, sheria na sera zinazowalenga,

» Kushiriki kikamilifu katika kufuatilia sera na mijadala inayohusu kupunguza umasikini

» Kuchangia katika maendeleo ya jamii na kuibana ipasavyo serikali na sekta binafsi katika masuala yanayohusu maendeleo ya jamii.

Maadili Yetu

Taasisi ya the Foundation imejiwekea maadili yafuatayo:

HAKI

Tutakuwa wa wazi, na wa kweli. Tutatoa taarifa zetu kwa yale tunayofanya huku tukizingatia utunzaji wa siri kwa taarifa zingine nyeti. Tutafanyakazi kuhakikisha kuwa huduma zetu zote hazibagui na zina msimamo wa usawa ndani yake.

Uadilifu

Taasisi ya the Foundation na wafanyakazi wake watatekeleza na pia watatetea uadilifu, kwa mapana yake yote, na kwenye shughuli zetu zote. Na kwamba hatutavumilia kwa namna yeyote ile aina yeyote ya rushwa ndani na nje ya Taasisi.

Heshima

Tutakuza na kuendeleza utamaduni ambapo wale wote tunaowasiliana nao watapa huduma kwa utaalamu wa juu, adabu na heshima wakati wote. Tutajitahidi kujenga uwezo wa wale wote wanaohusiana na Taasisi, kupitia shughuli zetu mbalimbali.

Ubora

Tutaendeleza sifa yetu kwa kuzingatia utendaji na utamaduni wa ubora uliotukuka, umahiri na utaalamu. Tutajitahidi kufikia na kuonyesha viwango vya juu vya kuaminika, uhodari na utendaji wa hali ya juu..

Kujifunza

Tutajenga mazingira ambayo yanathamini kujifunza na kubadilishana uzoefu

Foundation inaendeshwa na Sekretarieti na kutawaliwa na Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Wajumbe. Inalenga kuimarisha jumuia za kiraia ili zishiriki katika upunguzaji wa umaskini Tanzania, kama ilivyoonyeshwa kwenye sera za Serikali ya Tanzania. Uimarishaji huo ni kupitia ujenzi wa uwezo na kutoa ruzuku kwa jumuia za kiraia katika sehemu zote za Tanzania, ikilenga kwenye maeneo manne ya maudhui: sera, utawala, uimarishaji wa utetezi na mitandao ya usalama kwa walio katika hatari ya kudhurika. Utoaji wa ruzuku unaifanya Foundation iwe ya kipekee na tofauti, ukiifanya iwe tofauti na asasi zote za ujengaji wa uwezo Tanzania.

Foundation hailengi kuziwakilisha jumuia za kiraia au kuzungumza kwa niaba yake ila kujenga uwezo wa jumuia za kiraia katika namna ya uratibu zikiwa na viwango vya juu vya uwajibikaji, uwazi, ubora na maudhui.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Kuhusu sisi