Utoaji wa Ruzuku

 Foundation inatoa ruzuku yenye lengo la kuziwezesha Asasi za Kiraia zinazowajengea uwezo wananchi hasa masikini na walio pembezoni na makundi mengine yaliyo katika hatari ya kuathirika zaidi ili makundi hayo yaweze kushiriki katika mipango ya maendeleo na kupunguza umasikini.


Fomu za maombi ya ruzuku zinapatikana ofisini Foundation au kwa kupakua katika tovuti yetu.


Aina za ruzuku zitolewazo:
.Ruzuku ndogo 7,5000,000/-
Ruzuku ya kati 45,000,000/- kwa mwaka mmoja na 135,000,000/- kwa miaka mitatu.
Ruzuku kubwa 150,000,000/- kwa mradi wa mwaka mmoja na 450,000,000/- kwa mradi wa miaka mitatu.
Maeneo yanayofadhiliwa na Foundation.


Foundation itafadhili maombi yote ambayo yamelenga kufanya shughuli mbali mbali k katika maeneo lengwa yafuatayo:
Ushiriki katika utungaji wa sera na ufuatiliaji wake :Kuwezesha wananchi kushiriki na  kufuatilia utekelezaji wa sera katika kuimarisha utoaji wa huduma.


Kuimarisha Utawala bora na haki za kiraia: Kuwezesha wananchi kutambua haki zao na majukumu yao na kusimamia uwajibikaji katika matumzi ya rasilimali za umma


Kuimarisha uwezo wa Asasi za Kiraia: Kuhakikisha Asasi za kiraia zinakuwa nguzo imara katika kuleta uwajibikaji.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.