Pwani yatakiwa kutenga bajeti za walemavu

Madiwani wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini, mkoani Pwani, wametakiwa kuweka kipaumbele katika bajeti kwa makundi ya watu wenye ulemavu kwa lengo la kuyapatia uwezo wa kujitegemea wenyewe badala ya kutegemea wafadhili.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Shirika limalojishughulisha na mambo ya Vijana la YPC, Israel Ilunde, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Viziwi (CHAVITA) wilaya ya Kibaha Vijijini kwa Ufadhili wa The Foundation for Civil Society.

Ilunde anasema makundi hayo yamekuwa tegemezi kutokana na kutopewa kipaumbele kwenye bajeti inayoandaliwa na halmashauri  hiyo, hali inayowafanya waendelee kuwa ombaomba huku wakionyesha kuwa na uwezo wa kumudu maisha yao endapo wangepaiwa fedha za kuinua miradi yao.

Mkurugenzi huyo ameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuangalia uwezekano wa kukabiliana na suala hilo, kwani kundi hilo kila mmoja ana fani yake, hivyo wakiwezeshwa wanaweza kujitegemea.

Mwezeshaji Samweli Stanley, amesema ni vema wananchi wote bila kujali walemavu na wasio walemavu wakashirikishwa katika mipango ya maendeleo, ili kufahamu kinachofanywa na serikali yao, hali ambayo itawaondolea malalamiko.

Katibu wa CHAVITA Wilaya ya Kibaha, Mussa Khalid,ameweleza washiriki hao kwamba asasi yao imekuwa ikipigania utoaji wa elimu kwa makundi hayo kwa lengo la kuwapatia fursa ya kutambua nafasi yao.

Asasi Bagamoyo yawezeshwa kuibua wanachama hai

Mwana ruzuku wetu, asasi ya Bagamoyo Youth Information Centre (BAYOICE) sasa inajivunia kuweza kujipatia wanachama hai – siri kubwa ikiwa ni kuweza kuwabadilisha wanachama ‘goigoi’ kupitia mafunzo ya kuimarisha uendeshaji wa asasi waliyotoa kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society.

BAYOICE ni asasi inayoongozwa na vijana kwa nia ya kupanua wigo wa fursa za kiuchumi na kuboresha huduma za kijamii ili kuchangia jitihada za kupunguza umasikini na kuongeza kipato kwa wakazi wa wilaya ya Bagamoyo.

BAYOICE iko katika kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, na imekuwa ikijishughulisha katika kusaidia jamii juu ya changamoto mbalimbali zinazosababisha maendeleo kurudi nyuma.

Mwenyekiti wa BAYOICE, Ally Juma anasema: “Mafunzo yaliyofadhiliwa na Foundation yameleta mabadiliko makubwa katika asasi yetu na kuwawezesha wanachama wetu kutambua majukumu yao na kuboresha mfumo wa utendaji wa kazi tofauti na awali ambapo utendaji wao haukuwa mzuri”.

Juma anasema, wengi wao walikuwa hawawezi kujitolea katika utendaji wa kazi kwa ajili ya kuisaidia jamii mpaka kwanza wapewe posho.

Mbali ya kuwa tunafanya kazi na viongozi wa serikali kupitia halmashuri ya Wilaya, tumeweza kushirikiana na taasisi binafsi, shule za sekondari na msingi katika utojia wa elimu ya mafunzo mbalimbali kulingana na changamoto ambazo zinaikabili jamii.
Mwanachama wa asasi hiyo Josephine Jonasi anasema: “Nimeweza kuwa na upeo katika uandishi wa mradi baada ya kuwa nimepata mafunzo, sasa nafahamu namna ya kuandaa mradi bila kutegemea msaada kutoka kwa kiongozi wetu.”
“Pia katika kipengele cha sera ya taifa ya maendeleo ya vijana nimeweza kuitambua sera hiyo - hasa katika vile vipengele muhimu ambavyo vinatetea vijana na kutimiza wajibu wangu kama kijana ili kuisaidia jamii katika kuleta maendeleo,” anasema Josephine.

Juma anasema kutokana na uhamasishaji wa mafunzo wanachama wameweza kubuni miradi mbalimbali na hivyo kuweza kutatua matatizo tofauti kama vile ulipaji wa pango, gharama za umeme, na hata kujipatia nauli wakati wa kwenda kuendesha semina za mafunzo vijijini bila ya kutegemea na kusubiri ruzuku kutoka Foundation.
Anasema wanachama wamekuwa wakichangishana fedha kwa ajili ya kuendeleza mfuko wa asasi ambao pia unasaidia kuwalipia ada ya shule watoto walio katika mzingira magumu.

Asasi pia imeweza kujiendesha yenyewe kwa kuwa tayari imejengewa uwezo katika kuunda mpango mkakati, na wanachama tayari wamefahamu maana yake na wanatumia fursa hiyo kuaandaa mipango kazi mipya pasipo kumsubiri tena mwezeshaji.
Latifa Rashidi, ni mmoja wa wanuifikaji kupitia mafunzo hayo, anasema: “ilikuwa ni kazi ngumu kwangu kusimama na kujielezea mbele ya mkusanyiko wa watu, lakini sasa ninajiamini kwa kile ninachofikiria kuchangia kama mchango wa mawazo yangu”.

Anaongeza kuwa sasa asasi ina uwezo wa kufanya kazi zake katika jamii bila yao kama wanachama kuomba posho. Pia mafunzo yamemfanya atambue kuwa ni wajibu wake kuyaweka maslahi ya jamii mbele kwa kushilia dhana ya uwajibikaji.

Mwanachama wa asasi, Joseph Peter anasema kutokana na mafunzo wanachama wameweza kuondoa tofauti zao na hata kuondoa vijiashiria vya kuwepo kwa migogoro pindi wanachama wengine walipokuwa kukitegea katika utendaji.

Asasi imeweza kuwa karibu zaidi na jamii kutokana na wanachama wake wengi kutambua namna ya kuboresha maelewano na jamii inayowazunguka na hata kuwahamasisha wanachama wapya kujiunga kwa kuzingatia moyo wa kujitolea.

 Dorisi Kalemwa ambaye ni mwanachama asasi anasema mafunzo yamemhamasisha kuisambaza elimu hata kwa vijana wengine ambao hawakupata fursa kama ya kwakwe.


Aidha, BAYOICE sasa imeondokana na wimbi la kujikuta ikiendeshwa na watu wachache tu waliomo katoka jopo la viongozi na kubadilika kuwa asasi jumuishi. Salama Kassimu ambaye pia amenufaika na mafunzo anasema: “Kupitia mafunzo sasa wanachama tumekuwa na uelewa wa kuendesha asasi tofauti na hapo awali ambapo tulikuwa tunategemea viongozi wetu tu ndio wafanye kila kitu kwa niaba yetu. Sasa dhana ya uanachama hai imeweza kijidhihirisha na kujikita miongoni mwetu.”
   

Watoa Huduma wafundishwa lugha ya Alama

Zaidi ya watoa huduma 50 wakiwemo askari, polisi, walimu, wauguzi na madaktari kutoka tarafa za Mlimba na Kidatu wamepewa elimu ya lugha za alama.

Mratibu wa mradi wa mafunzo ya alama wilayani Kilombero Elizabeth Rutha, alisema mradi huo wenye lengo la kuwafikia watoa huduma 137, umeanza na tarafa hizo na baadae tarafa za Mngeta na Ifakara.

Alisema mradi huo unaofadhiliwa na Foundation for Civil Society unatarajiwa kugharimu sh milioni 42.7.

Rutha alisema wameaamua kutoa mafunzo hayo kwasababu viziwi wengi wanapata tabu wawapo katika vituo vinavyotoa huduma za kijamii kutokana na kutokuwa na wataalamu wa lugha ya alama na wakalimani.

Kwa upande wao, waliopewa mafunzo hayo wamekipomgeza Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Kilombero kwa kuwapa mafunzo hayo kwani awali walikuwa katika wakati mgumu wa kuwasiliana na viziwi kwa kutofahamu njia za mawasiliano.

Hata hivyo, wameshauri mafunzo hayo kutolewa mara kwa mara,ili wawe na uelewa mpana zaidi wa lugha hiyo.

Walemavu Urambo walalamika kukosa elimu

Zaidi ya asilimia tisini ya walemavu wote wilayani Urambo mkoani Tabora hawana elimu kutokana na kukosa fursa na kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya kupata elimu.

Wilaya ya Urambo yenye watu wenye ulemavu zaidi ya 900 inafanya watu wenye ulemavu wasio na elimu zaidi ya watu 860.

Akizungumza katika mafunzo ya watu wenye ulemavu wa macho, Mwenyekiti wa Chama cha Wasiiona wilayani Urambo, Daniel Mwita, alisema kwa kukosa elimu walemavu wanakuwa katika wakati mgumu huku wengi wakiishi maisha yasiyo mazuri.
“Wengi wetu hasa wanaoishi maeneo ya vijijini hali yao kimaisha sio nzurio kwani wao wana matatizo,” alisema.

Akifungua mafunzo hayo, Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Noel Ndallu, alisema serikali inawathamini watu wenye ulemavu na ndiyo maana miundombinu inawekwa kwaajili yao ingawa jitihada bado hazitoshi.

Katika risala yao iliyosomwa na msaidizi wao, Focus Magwesela watu wenye ulemavu walisema wana mpango mkubwa katika kulitetea Taifa maendeleo kwa vile wana uwezo wa kufanya kazi.

Magwesela alisema pamoja na kuwa na ulemavu lakini wenye ulemavu wana haki ya kupata mahitaji ya msingi mfano elimu na mengineyo kama watu ambao hawana ulemavu.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanahudhuriwa na watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali yakiwa yameandaliwa na Chama cha Wasioona wilayani Urambo na kufadhiliwa na Foundation for Civil Society.

Asasi Morogoro zapongeza jitihada za Foundation

Asasi zisizo za kiserikali mkoani Morogoro zimelipongeza Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) kwa jitihada zake za kuelimisha wananchi na kutambua wajibu na majukumu yake katika kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa  na katibu wa Kijogoo Group for Community Development, Bw. Ramadhan Said juu ya mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuleta mabadiliko nchini katika sekta mbalimbali.

Alisema mashirika mengi yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakifadhiliwa na Foundation yamekuwa chachu kubwa katika kuibua kero katika maeneo yao ikiwa pamoja na kuishauri serikalimara baada ya tafiti zao kukamilika.

Bw.Said alisema kuwa shirika lake ni miongoni mwa mashirika ambayo yamefadhiliwa na Foundation kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kuwafikia jamii katika maeneo yao.

Bw.Said alisema kuwa kutokana na elimu hiyo sasa jamii imetambua umuhimu wa kusimamaia miradi yao ikiwa pamoja na kufuatilia mapato na matumizi ya rasilimali za umma katika maeneo yao.

Hata hivyo alidai kuwa jamii haina uelewa juu ya haki na wajibu wao katika kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao, hali ambayo kwa sasa jamii imepata uelewa na hivyo kumudu kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo kwa waledi mkubwa.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari