Mdahalo wa Asasi wasisitiza mustabakali wa Tanzania unategemea kilimo

Wadau wa maendeleo mkoani Mtwara wameiomba serikali kuwekeza zaidi katika kilimo na kubuni mbinu za kukuza sekta ya hiyo ili kuwavutia vijana kubaki vijijini badala ya kukimbilia mjini na kukosa ajira.

Wito huo umetolewa katika mdahalo wa sera na mstakabali wa nchi kwa miaka 20 ijayo, ulioandaliwa na shirika la Society for International Development (SID) na kufadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS).

Akitoa tathmini ya mdahalo, Katibu Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mtwara (MTWANGONET) Fidea Luanda, amesema mdahalo huo ni sehemu ya utekelezaj wa mradi wa midahalo ya kujadili mustakabali wa nchi katika miaka 20 ijayo ambapo Mtwara ni moja kati ya mikoa tisa iliyopata nafasi hiyo.


Uelewa wa sheria za ardhi kupunguza migogoro Morogoro

Migogoro ya ardhi inatokana na wananchi kutojua sheria za ardhi na hata kutohusishwa katika mabaraza ya ardhi yaliyopo katika vijiji vyao.

Mwenyekiti wa Melela Farmers Development Foundation (MEFADEO), Zaka Shomari amesema migogoro mingi hutokea kwa sababu ya wananchi kutohusishwa katika mikutano inayohusiana na ardhi na kutojua sheria.

Ameyasema haya hivi karibuni katika mafunzo ya siku nne juu ya Sheria ya Ardhi ya vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999 yaliyofadhiliwa na The Foundation for Civil Society juu ya masuala ya ardhi.

Amesema kuwa, mkoa wa Morogoro unaongoza kwa migogoro ya ardhi hasa kwa wafugaji na wakulima suala hilo linatishia amani na kusababisha watu wengi kupoteza maisha yao na hata mali.

“Haya mafunzo tuliyoyatoa yatawasaidia wananchi katika suala la migogoro ili kila mtu ajue haki yake ya msingi,” says Shomari.
Afisa Maendeleo wa kata ya Melela mkoa wa Morogoro, Bi. Gloria Mundo amesema kuwa mafunzo haya yatawajenga wananchi  katika kujua haki zao za msingi katika suala la migogoro ya ardhi.

Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa migogoro ya ardhi kwa wakulima na wafugaji  lakini mafunzo haya yakiwa yanatolewa mara kwa mara wananchi wataelimika na watajua wajibu wao.

Wasioona wahitaji Katiba Mpya ya nukta nundu

Walemavu wasiiona katika halmashauri ya jiji la Tanga wanaiomba serikali kuangalia uwezekano utakaowapatia nakala za Katiba ya nchi katika mfumo wa maandishi ya nukta nundu (Braille) ili kundi hilo lipate fursa pana na uhuru wa kusoma.

Walitoa ombi hilo kwa wakati tofauti  walipozungumzia matokeo ya ushiriki wao kwenye mafunzo maalum ya kujengewa uwezo kuhusu Katiba ya Tanzania na Rasimu (Marekebisho) ya Katiba Mpya.

Wamesema wanapongeza jitihada zilizofanywa na wadau, kuhakikisha kundi la wasioona nchini wanapata fursa ya kutoa maoni yao kama Watanzania wengine kwa kusomewa maandishi na watu wanaaona.

Hata hivyo wamedai kwamba mbinu hiyo ya ubunifu, siyo ya kudumu na inawanyima uhuru wa kuisoma katiba kwa kina ili kuielewa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona wilayani Tanga, Akida Ally amesema mafunzo hayo yamewapa mwangaza wa kuelewa kuhusu Katiba ya Tanzania ambayo yamefadhiliwa na The Foundation for Civil Society.

“Tunashukuru sana kupata mafunzo  kwasababu yameondoa giza kwenye ufahamu wa kundi hili maalum, kabla ya mafunzo haya idadi kubwa ya wanachama hatukuwa na uelewa wowote kuhusu mambo yaliyomo kwenye katiba,”  amesema.

Ameongeza kuwa “tumesomewa kwa muhtasari na kufafanuliwa msingi wa mambo yote muhimu yaliyomo kwenye Katiba ..tumejua utendaji wa serikali, haki za raia, makundi maalum na kubwa zaidi tumeweza kutoa maoni yetu kama walemavu na tunashukuru yameweza kufanyiwa kazi katika mchakato wa mabadiliko unaoendelea.”

Elizabeth Bakari ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo amesema sasa amejitambua, amejua haki na wajibu wake.

Pia, amesema amepata ujasiri mkubwa wa kuthubutu kushirikiana na makundi mengine kwenye mtaa anaoishi ili kuchochea harakati za maendeleo kwenye jamii yake.

Kwa upande wake Mtindi Goshi , amesema amepatiwa nakala za rasimu hiyo kama wananchi wengine .
Ametaja changamoto inayowakabili ni kukosa wasomaji hasa kwa muda wa ziada.

Amesema wao wanahitai mno wasomaji ili kuendelea kujifunza mambo yaliyomo, hasa kwa kuzingatia mijadala inayoendelea bungeni na katika makongamano ya kitaifa.

“Wakati unaposomewa huwezi kukumbuka kila kitu na pia sio kila wakati mtu asiyeona anaweza kuwa karibu na msomaji kwa karibu na msomaji wa nakala zilizopo sasa.



Wananchi Morogoro watakiwa kumiliki ardhi kisheria

Wananchi wa kata ya Hembeti mkoani Morogoro wameshauriwa kumiliki ardhi kisheria ili kuepukana na migogoro isiyo ya lazima.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni katika kijiji cha Mkindo na Mwanasheria wa Kituo cha usaidizi wa Sheria Morogoro Paralegal Centre (MPLC), Sabas Casmir wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mafunzo ya siku moja kuhusiana na sheria ya ardhi ya mwaka 1999 kifungu no. 4&5 yaliyofadhiliwa na The Foundation for Civil Society.

Casmir amesema migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na wananchi wenyewe kutofuata sheria za kumiliki ardhi na kushindwa kufuata utaratibu wa kutumia vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Ameongeza iwapo wananchi hao watatumia kikamilifu baraza la ardhi la kijiji ambalo linahusika na usuluhishi na pamoja na baraza la ardhi la kata, ana uhakika migogoro hiyo itapungua kwa kiasi kikubwa kama siyo kumalizika.

Naye mwenyekiti wa baraza la kata ya Hembeti, Mahunda Mziwanda amesema baraza la kata yake limekuwa likipokea changamoto nyingi za ardhi kutokana na mabaraza ya kijiji kutwaa madaraka ya kutoa maamuzi badala ya kusuluhisha.

Mziwanda amesema imefikia mahali mabaraza hayo ya kijiji kutoza faini hadi ya shilingi laki moja, huku wakijua wanakiuka sheria na hivyo kusababisha kesi nyingi kurundikana katika mabaraza hayo.

 

Asasi Kagera kukabiliana na changamoto za wazee

Wazee mkoani Kagera wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, ukosefu wa vipato na kukosekana kwa mfuko wa jamii wa wazee.

Haya yamesemwa na Mwanasheria wa Shirika la Saidia wazee Karagwe (SAWAKA), Ruth Hole, wakati alipokuwa anaendesha semina kuhusiana na sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 kifungu no 4&5 iliyofadhiliwa na The Foundation for Civil Society.

Hole amesema, wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, ukosefu wa kipato na kukosekana kwa mfuko wa jamii wa wazee ambako kumesababisha maendeleo ya Taifa kurudi nyuma, ikiwa pamoja na wazee wengi kutojua taratibu ambazo zingeweza kutatua matatizo.

Amesema tatizo kubwa ni wazee wengi kutojua kusoma na kuandika,  ambako mara kwa mara vipato vyao vinapungua wakati wakuuza mazao kwa kupewa fedha kidogo zisizostahili na mauzo hayo.

Ameeleza kwamba wazee wengi wanakuwa na hali ngumu ya maisha kutokana na kutojishughulisha, ikiwa ni pamoja na vijana wao kuishi vijiweni, kunywa pombe na utunmiaji wa madawa ya kulevya, hivyo kuwapa mzigo mkubwa wazazi wazazi wao kwa kuwategemea kwa mahitaji yao.




Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari