Wafanyakazi wa FCS waagwa

Wafanyakazi 8 wa FCS wamefanyiwa hafla ya kuagwa kufuatia muda wao wa utumishi katika shirika hili kuisha. Wafanyakazi walioagwa ni pamoja n; Tadeo Lupembe (Meneja wa afaedha na Uendeshaji), Marilyn Elinewinga (Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani), Vicent Nalwendela (Mkuu wa Mawasiliano), Nestory Mhando (Afisa Mwandamizi-Ruzuku), Kemilembe Mpinga (Afisa Msaidizi- Ruzuku), Gladys Mkuchu (Afisa -Mawasiliano), Chrispina Mwacha (Afisa-Mjenzi Uwezo) and Kasoga Kasika (Mkaguzi wa Ndani).

 Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga alisema, FCS inajivunia utendaji wao wa kazi na kwamba inaamini wanaondoka FCS wakiwa wameiva kiutendaji na hivyo wanakwenda kuwa mabalozi wazuri wa shirika hili. Tadeo Lupembe (Finance &Operation Manager), Marilyn Elinewinga (Head of Internal Audit) Vicent Nalwendela (Head Communications), Nestory Mhando (Senior Program officer-Grants), Kemilembe Mpinga (Assistant Program Officer-Grants), Gladys Mkuchu (Program Officer-Cumminucations), Chrispina Mwacha (Program Officer-Capacity Development) and Kasoga Kasika (Internal Auditor).

Halfa hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wote wa FCS na ilifanyika zilipo ofisi za FCS Ijumaa ya Februari 3, 2017. Kuondoka kwa wafanyakazi hao kunatokana na kumalizika kwa muda wao wa utendaji katika FCS pamoja na kukabiliwa na majukumu mengine.

FCS washeherekea Jumanne ya Kutoa kwa mafanikio

Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society, leo limeadhimisha siku ya Jumanne ya Kutoa maarufu kama ‘Giving Tuesday’ kwa kutoa misaada mbalimbali katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyoko jijini Dar es Salaam.

Shughuli hii inaadhimishwa kila Jumanne ya mwisho ya mwezi Novemba duniani kote na kwa hapa Tanzania, hii ni mara ya kwanza kuadhimishwa. Msingi ya shughuli hii ni jamii kujitolea kusaidia katika huduma za jamii na hasa kuchangia wasiojiweza, na kufanya kazi zingine zinazogusa watu wenye uhitaji.

Akizungumza katika Shughuli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga alisema shirika lake kwa kutambua umuhimu wa mashirika, makampuni na watu binafsi katika jamii, limeamua kuleta utamaduni huu hapa nchini na hii inapaswa kuwa ni moja ya shughuli zinazotakiwa kufanywa na kila shirika walau mara moja katika mwaka. Mkurugenzi huyo alisema wafanyakazi wa shirika hilo waliamua kuchangia shughuli hii kwa asilimia moja ya mishahara yao kwa miezi sita na kisha kampeni hii nzima imesaidia kukarabati choo kimoja kinatumiwa na wanafunzi wa shule hii. Pia kupitia kampeni hii wanafunzi wamepewa mabegi ya kubebea daftari, magodoro, foronya, vyakula na vitabu.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala kutoka katika Wizara ya Elimu, Pancras Steven alisema anashukuru kwa mchango huu wa FCS na kwamba shirika hili limeonesha kuwa liko makini na kwamba linajali maendeleo ya kila watu na hasa walio na uhitaji zaidi.

Kazi hii mliyofanya ni kubwa mno hivuo nawapongeza. Nitumie name nafasi hii kuwaomba Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia katika majukumu ya maendeleo katika jamii. Kwa kufanya hivi mnasaidia sana kuhamasisha jamii nasi kama serikali tunaungana nanyi,” alisema.

Awali akizungumza kwa niaba ya Shule hiyo Mawalimu Mkuu wa Uhuru Mchanganyiko, Bi. Anna Mshana alisema anaishukuru FCS kwa kuichagua shule yake kwa kuwa kweli ni shule yenye uhitaji mkubwa na kwamba wanafunzi wanaosoma katika shule yake ni tofauti na wale wanaosoma katika shule zingine.

Tunakushukuruni sana kwa kazi hii kubwa na kwa michango yenu. Sisi tumefarijika sana na hasa kwa ninyi kuchagua kuja katika shule yetu kutupa misaada. Tunaomba msisite kuja siku nyingine,” alisema.

Shughuli hiyo iliambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii Barnaba na Miriam, msanii mwenye uoni hafifu. Pia kulikuwa na kazi za kupanda miti, kufanya usafi, kupaka rangi na michezp mbalimbali na watoto.

 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, mwanzo wa shughuli hii unamaanisha itaendelea tena hapo mwakani. “Tunajipanga kufanya kubwa sana mwakani na maandalizi yake tutayaanza mapema,” anasema.

FCS waendesha mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana Dar es Salaam

 Pichani ni Bi. Nasim Losai (Afisa Miradi wa FCS) akifungua mafunzo hayo

Shirika la ‘Foundation for Civil Society’ (FCS) limeendesha mafunzo ya siku tatu ya Biashara, Fursa, Taratibu na Sheria za kufanya Biashara kwa Vijana ndani ya soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mafunzo hayo yamezinduliwa leo Jumatatu Novemba 21, 2016 katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.

Vijana hawa wanapewa mbinu za ujasiliamali na namna ya kumudu kushindana ikiwa ni hatua ya kutambua mtangamano wa Afrika Mashariki, pamoja na kumjengea uwezo kijana wa Tanzania ili aweze kumudu ushindani wa wenzake katika nchi zinazounda jumuiya hii.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Afisa Miradi kutoka FCS, Nasim Losai alisema kuwa, FCS inatambua jitihada za serikali ya Tanzania katika kuwawezesha vijana wa Tanzania na katika kubaini hilo, shirika hilo linaelewa changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na hivyo mafunzo hayo ni moja ya mbinu za kupunguza changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania.

Bi. Losai alieleza pia kuwa, mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu na yatashirikisha watoa mada mbalimbali wenye uzoefu katika maeneo yao na hasa yale ambayo ynaonesha fursa katika nchi za Afrika Mashariki.

Ni dhamira yetu kuona vijana hawa wajifunze na wakitoka hapa wawe walimu kwa wenzao huko wanakoishi. Tungependa kuwa nao wengi zaidi lakini hawa waliopo wanawawakilisha wenzao na imani yetu ni kuwa elimu hii ya fursa wanayoipata hapa leo wataitumia na itawasaidia katika kubadili maisha yao,” alisema. 

Picha ya pili ni ya Mwendeshaji Mkuu wa Mafunzo hayo Bi. Losai katikati akiwa na washiriki wengine.

NAIBU WAZIRI POSI AZINDUA TAMASHA LA TANO LA WATU WENYE ULEMAVU JIJINI DAR

 

Naibu Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi leo amezindua tamasha la tano ya watu wenye ulemavu nchini, Tamasha lililoandaliwa kwa udhamini wa Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation of Civil Society, lililofanyika katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.

Dk. Posi amebainisha katika Tamasha hilo kuwa, serikali ipo karibu na watu wenye ulemavu na kwamba sheria iliyopitishwa mwaka 2010, kuhusu watu wenye ulemavu imepitishwa na kwamba ni jukumu la jamii nzima kushirikiana katka kutoa haki sawa kwa wananchi wote wakiwemo walemavu.

Dk. Posi alifafanua kuwa, changamoto zinazowakabili walemavu hapa nchini ni nyingi lakini pia serikali inazitambua, inazichambua na inazifanyia kazi kwa kadri uwezo unapopatikana.

Kabla ya hotuba ya Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society, Fransis Kiwanga alifafanua kuwa, shirika analoliongoza kwa kutambua umuhimu wa kuwawezesha walemavu hapa nchini, liliona ni busara kuchangia kuwepo kwa tamasha hili na kwamba ni faraja kwa shirika hili kuona maisha na hali ya walemavu hapa nchini inabadilika.

Tunaipongeza serikali kwa kazi kubwa inayofanya, tunaipongeza sana katika suala zima la kupinga rushwa, Tunaipongeza katika kuhakikisha kunakuwepo mabadiliko ya utendaji pamoja na utoaji huduma kwa wananchi,” Mkurugenzi huyo alisema na kuongeza kuwa, shirika lake kwa kutambua haki mbalimbali za walemavu na hali halisi ya maisha hapa nchini, linaiomba serikali kuhakikisha kuwa inakuwa karibu na watu wenye mahitaji maalum ili nao wajione kuwa ni raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu.

Tamasha hili linalounganisha wawakilishi wa watu wenye mahitaji maalum kutoka pane zote za Tanzania, linafanyika kwa siku mbili na likihusisha wawakilishi wapatao 150 kutoka katika mikoa yote nchini Tanzania na linafanyika hapa jijini Dar es Salaam kwa siku mbili.

 

 

 

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari