FCS washeherekea Jumanne ya Kutoa kwa mafanikio

Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society, leo limeadhimisha siku ya Jumanne ya Kutoa maarufu kama ‘Giving Tuesday’ kwa kutoa misaada mbalimbali katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyoko jijini Dar es Salaam.

Shughuli hii inaadhimishwa kila Jumanne ya mwisho ya mwezi Novemba duniani kote na kwa hapa Tanzania, hii ni mara ya kwanza kuadhimishwa. Msingi ya shughuli hii ni jamii kujitolea kusaidia katika huduma za jamii na hasa kuchangia wasiojiweza, na kufanya kazi zingine zinazogusa watu wenye uhitaji.

Akizungumza katika Shughuli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga alisema shirika lake kwa kutambua umuhimu wa mashirika, makampuni na watu binafsi katika jamii, limeamua kuleta utamaduni huu hapa nchini na hii inapaswa kuwa ni moja ya shughuli zinazotakiwa kufanywa na kila shirika walau mara moja katika mwaka. Mkurugenzi huyo alisema wafanyakazi wa shirika hilo waliamua kuchangia shughuli hii kwa asilimia moja ya mishahara yao kwa miezi sita na kisha kampeni hii nzima imesaidia kukarabati choo kimoja kinatumiwa na wanafunzi wa shule hii. Pia kupitia kampeni hii wanafunzi wamepewa mabegi ya kubebea daftari, magodoro, foronya, vyakula na vitabu.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala kutoka katika Wizara ya Elimu, Pancras Steven alisema anashukuru kwa mchango huu wa FCS na kwamba shirika hili limeonesha kuwa liko makini na kwamba linajali maendeleo ya kila watu na hasa walio na uhitaji zaidi.

Kazi hii mliyofanya ni kubwa mno hivuo nawapongeza. Nitumie name nafasi hii kuwaomba Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia katika majukumu ya maendeleo katika jamii. Kwa kufanya hivi mnasaidia sana kuhamasisha jamii nasi kama serikali tunaungana nanyi,” alisema.

Awali akizungumza kwa niaba ya Shule hiyo Mawalimu Mkuu wa Uhuru Mchanganyiko, Bi. Anna Mshana alisema anaishukuru FCS kwa kuichagua shule yake kwa kuwa kweli ni shule yenye uhitaji mkubwa na kwamba wanafunzi wanaosoma katika shule yake ni tofauti na wale wanaosoma katika shule zingine.

Tunakushukuruni sana kwa kazi hii kubwa na kwa michango yenu. Sisi tumefarijika sana na hasa kwa ninyi kuchagua kuja katika shule yetu kutupa misaada. Tunaomba msisite kuja siku nyingine,” alisema.

Shughuli hiyo iliambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii Barnaba na Miriam, msanii mwenye uoni hafifu. Pia kulikuwa na kazi za kupanda miti, kufanya usafi, kupaka rangi na michezp mbalimbali na watoto.

 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, mwanzo wa shughuli hii unamaanisha itaendelea tena hapo mwakani. “Tunajipanga kufanya kubwa sana mwakani na maandalizi yake tutayaanza mapema,” anasema.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari FCS washeherekea Jumanne ya Kutoa kwa mafanikio