FCS waendesha mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana Dar es Salaam

 Pichani ni Bi. Nasim Losai (Afisa Miradi wa FCS) akifungua mafunzo hayo

Shirika la ‘Foundation for Civil Society’ (FCS) limeendesha mafunzo ya siku tatu ya Biashara, Fursa, Taratibu na Sheria za kufanya Biashara kwa Vijana ndani ya soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mafunzo hayo yamezinduliwa leo Jumatatu Novemba 21, 2016 katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.

Vijana hawa wanapewa mbinu za ujasiliamali na namna ya kumudu kushindana ikiwa ni hatua ya kutambua mtangamano wa Afrika Mashariki, pamoja na kumjengea uwezo kijana wa Tanzania ili aweze kumudu ushindani wa wenzake katika nchi zinazounda jumuiya hii.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Afisa Miradi kutoka FCS, Nasim Losai alisema kuwa, FCS inatambua jitihada za serikali ya Tanzania katika kuwawezesha vijana wa Tanzania na katika kubaini hilo, shirika hilo linaelewa changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na hivyo mafunzo hayo ni moja ya mbinu za kupunguza changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania.

Bi. Losai alieleza pia kuwa, mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu na yatashirikisha watoa mada mbalimbali wenye uzoefu katika maeneo yao na hasa yale ambayo ynaonesha fursa katika nchi za Afrika Mashariki.

Ni dhamira yetu kuona vijana hawa wajifunze na wakitoka hapa wawe walimu kwa wenzao huko wanakoishi. Tungependa kuwa nao wengi zaidi lakini hawa waliopo wanawawakilisha wenzao na imani yetu ni kuwa elimu hii ya fursa wanayoipata hapa leo wataitumia na itawasaidia katika kubadili maisha yao,” alisema. 

Picha ya pili ni ya Mwendeshaji Mkuu wa Mafunzo hayo Bi. Losai katikati akiwa na washiriki wengine.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari FCS waendesha mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana Dar es Salaam