Uelewa wa sheria za ardhi kupunguza migogoro Morogoro

Migogoro ya ardhi inatokana na wananchi kutojua sheria za ardhi na hata kutohusishwa katika mabaraza ya ardhi yaliyopo katika vijiji vyao.

Mwenyekiti wa Melela Farmers Development Foundation (MEFADEO), Zaka Shomari amesema migogoro mingi hutokea kwa sababu ya wananchi kutohusishwa katika mikutano inayohusiana na ardhi na kutojua sheria.

Ameyasema haya hivi karibuni katika mafunzo ya siku nne juu ya Sheria ya Ardhi ya vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999 yaliyofadhiliwa na The Foundation for Civil Society juu ya masuala ya ardhi.

Amesema kuwa, mkoa wa Morogoro unaongoza kwa migogoro ya ardhi hasa kwa wafugaji na wakulima suala hilo linatishia amani na kusababisha watu wengi kupoteza maisha yao na hata mali.

“Haya mafunzo tuliyoyatoa yatawasaidia wananchi katika suala la migogoro ili kila mtu ajue haki yake ya msingi,” says Shomari.
Afisa Maendeleo wa kata ya Melela mkoa wa Morogoro, Bi. Gloria Mundo amesema kuwa mafunzo haya yatawajenga wananchi  katika kujua haki zao za msingi katika suala la migogoro ya ardhi.

Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa migogoro ya ardhi kwa wakulima na wafugaji  lakini mafunzo haya yakiwa yanatolewa mara kwa mara wananchi wataelimika na watajua wajibu wao.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Uelewa wa sheria za ardhi kupunguza migogoro Morogoro