Wasioona wahitaji Katiba Mpya ya nukta nundu

Walemavu wasiiona katika halmashauri ya jiji la Tanga wanaiomba serikali kuangalia uwezekano utakaowapatia nakala za Katiba ya nchi katika mfumo wa maandishi ya nukta nundu (Braille) ili kundi hilo lipate fursa pana na uhuru wa kusoma.

Walitoa ombi hilo kwa wakati tofauti  walipozungumzia matokeo ya ushiriki wao kwenye mafunzo maalum ya kujengewa uwezo kuhusu Katiba ya Tanzania na Rasimu (Marekebisho) ya Katiba Mpya.

Wamesema wanapongeza jitihada zilizofanywa na wadau, kuhakikisha kundi la wasioona nchini wanapata fursa ya kutoa maoni yao kama Watanzania wengine kwa kusomewa maandishi na watu wanaaona.

Hata hivyo wamedai kwamba mbinu hiyo ya ubunifu, siyo ya kudumu na inawanyima uhuru wa kuisoma katiba kwa kina ili kuielewa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona wilayani Tanga, Akida Ally amesema mafunzo hayo yamewapa mwangaza wa kuelewa kuhusu Katiba ya Tanzania ambayo yamefadhiliwa na The Foundation for Civil Society.

“Tunashukuru sana kupata mafunzo  kwasababu yameondoa giza kwenye ufahamu wa kundi hili maalum, kabla ya mafunzo haya idadi kubwa ya wanachama hatukuwa na uelewa wowote kuhusu mambo yaliyomo kwenye katiba,”  amesema.

Ameongeza kuwa “tumesomewa kwa muhtasari na kufafanuliwa msingi wa mambo yote muhimu yaliyomo kwenye Katiba ..tumejua utendaji wa serikali, haki za raia, makundi maalum na kubwa zaidi tumeweza kutoa maoni yetu kama walemavu na tunashukuru yameweza kufanyiwa kazi katika mchakato wa mabadiliko unaoendelea.”

Elizabeth Bakari ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo amesema sasa amejitambua, amejua haki na wajibu wake.

Pia, amesema amepata ujasiri mkubwa wa kuthubutu kushirikiana na makundi mengine kwenye mtaa anaoishi ili kuchochea harakati za maendeleo kwenye jamii yake.

Kwa upande wake Mtindi Goshi , amesema amepatiwa nakala za rasimu hiyo kama wananchi wengine .
Ametaja changamoto inayowakabili ni kukosa wasomaji hasa kwa muda wa ziada.

Amesema wao wanahitai mno wasomaji ili kuendelea kujifunza mambo yaliyomo, hasa kwa kuzingatia mijadala inayoendelea bungeni na katika makongamano ya kitaifa.

“Wakati unaposomewa huwezi kukumbuka kila kitu na pia sio kila wakati mtu asiyeona anaweza kuwa karibu na msomaji kwa karibu na msomaji wa nakala zilizopo sasa.Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Wasioona wahitaji Katiba Mpya ya nukta nundu