Wananchi Morogoro watakiwa kumiliki ardhi kisheria

Wananchi wa kata ya Hembeti mkoani Morogoro wameshauriwa kumiliki ardhi kisheria ili kuepukana na migogoro isiyo ya lazima.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni katika kijiji cha Mkindo na Mwanasheria wa Kituo cha usaidizi wa Sheria Morogoro Paralegal Centre (MPLC), Sabas Casmir wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mafunzo ya siku moja kuhusiana na sheria ya ardhi ya mwaka 1999 kifungu no. 4&5 yaliyofadhiliwa na The Foundation for Civil Society.

Casmir amesema migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na wananchi wenyewe kutofuata sheria za kumiliki ardhi na kushindwa kufuata utaratibu wa kutumia vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Ameongeza iwapo wananchi hao watatumia kikamilifu baraza la ardhi la kijiji ambalo linahusika na usuluhishi na pamoja na baraza la ardhi la kata, ana uhakika migogoro hiyo itapungua kwa kiasi kikubwa kama siyo kumalizika.

Naye mwenyekiti wa baraza la kata ya Hembeti, Mahunda Mziwanda amesema baraza la kata yake limekuwa likipokea changamoto nyingi za ardhi kutokana na mabaraza ya kijiji kutwaa madaraka ya kutoa maamuzi badala ya kusuluhisha.

Mziwanda amesema imefikia mahali mabaraza hayo ya kijiji kutoza faini hadi ya shilingi laki moja, huku wakijua wanakiuka sheria na hivyo kusababisha kesi nyingi kurundikana katika mabaraza hayo.

 

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Wananchi Morogoro watakiwa kumiliki ardhi kisheria