Asasi Kagera kukabiliana na changamoto za wazee

Wazee mkoani Kagera wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, ukosefu wa vipato na kukosekana kwa mfuko wa jamii wa wazee.

Haya yamesemwa na Mwanasheria wa Shirika la Saidia wazee Karagwe (SAWAKA), Ruth Hole, wakati alipokuwa anaendesha semina kuhusiana na sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 kifungu no 4&5 iliyofadhiliwa na The Foundation for Civil Society.

Hole amesema, wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, ukosefu wa kipato na kukosekana kwa mfuko wa jamii wa wazee ambako kumesababisha maendeleo ya Taifa kurudi nyuma, ikiwa pamoja na wazee wengi kutojua taratibu ambazo zingeweza kutatua matatizo.

Amesema tatizo kubwa ni wazee wengi kutojua kusoma na kuandika,  ambako mara kwa mara vipato vyao vinapungua wakati wakuuza mazao kwa kupewa fedha kidogo zisizostahili na mauzo hayo.

Ameeleza kwamba wazee wengi wanakuwa na hali ngumu ya maisha kutokana na kutojishughulisha, ikiwa ni pamoja na vijana wao kuishi vijiweni, kunywa pombe na utunmiaji wa madawa ya kulevya, hivyo kuwapa mzigo mkubwa wazazi wazazi wao kwa kuwategemea kwa mahitaji yao.
Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Asasi Kagera kukabiliana na changamoto za wazee