Pwani yatakiwa kutenga bajeti za walemavu

Madiwani wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini, mkoani Pwani, wametakiwa kuweka kipaumbele katika bajeti kwa makundi ya watu wenye ulemavu kwa lengo la kuyapatia uwezo wa kujitegemea wenyewe badala ya kutegemea wafadhili.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Shirika limalojishughulisha na mambo ya Vijana la YPC, Israel Ilunde, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Viziwi (CHAVITA) wilaya ya Kibaha Vijijini kwa Ufadhili wa The Foundation for Civil Society.

Ilunde anasema makundi hayo yamekuwa tegemezi kutokana na kutopewa kipaumbele kwenye bajeti inayoandaliwa na halmashauri  hiyo, hali inayowafanya waendelee kuwa ombaomba huku wakionyesha kuwa na uwezo wa kumudu maisha yao endapo wangepaiwa fedha za kuinua miradi yao.

Mkurugenzi huyo ameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuangalia uwezekano wa kukabiliana na suala hilo, kwani kundi hilo kila mmoja ana fani yake, hivyo wakiwezeshwa wanaweza kujitegemea.

Mwezeshaji Samweli Stanley, amesema ni vema wananchi wote bila kujali walemavu na wasio walemavu wakashirikishwa katika mipango ya maendeleo, ili kufahamu kinachofanywa na serikali yao, hali ambayo itawaondolea malalamiko.

Katibu wa CHAVITA Wilaya ya Kibaha, Mussa Khalid,ameweleza washiriki hao kwamba asasi yao imekuwa ikipigania utoaji wa elimu kwa makundi hayo kwa lengo la kuwapatia fursa ya kutambua nafasi yao.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Pwani yatakiwa kutenga bajeti za walemavu