Watoa Huduma wafundishwa lugha ya Alama

Zaidi ya watoa huduma 50 wakiwemo askari, polisi, walimu, wauguzi na madaktari kutoka tarafa za Mlimba na Kidatu wamepewa elimu ya lugha za alama.

Mratibu wa mradi wa mafunzo ya alama wilayani Kilombero Elizabeth Rutha, alisema mradi huo wenye lengo la kuwafikia watoa huduma 137, umeanza na tarafa hizo na baadae tarafa za Mngeta na Ifakara.

Alisema mradi huo unaofadhiliwa na Foundation for Civil Society unatarajiwa kugharimu sh milioni 42.7.

Rutha alisema wameaamua kutoa mafunzo hayo kwasababu viziwi wengi wanapata tabu wawapo katika vituo vinavyotoa huduma za kijamii kutokana na kutokuwa na wataalamu wa lugha ya alama na wakalimani.

Kwa upande wao, waliopewa mafunzo hayo wamekipomgeza Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Kilombero kwa kuwapa mafunzo hayo kwani awali walikuwa katika wakati mgumu wa kuwasiliana na viziwi kwa kutofahamu njia za mawasiliano.

Hata hivyo, wameshauri mafunzo hayo kutolewa mara kwa mara,ili wawe na uelewa mpana zaidi wa lugha hiyo.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Watoa Huduma wafundishwa lugha ya Alama