Walemavu Urambo walalamika kukosa elimu

Zaidi ya asilimia tisini ya walemavu wote wilayani Urambo mkoani Tabora hawana elimu kutokana na kukosa fursa na kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya kupata elimu.

Wilaya ya Urambo yenye watu wenye ulemavu zaidi ya 900 inafanya watu wenye ulemavu wasio na elimu zaidi ya watu 860.

Akizungumza katika mafunzo ya watu wenye ulemavu wa macho, Mwenyekiti wa Chama cha Wasiiona wilayani Urambo, Daniel Mwita, alisema kwa kukosa elimu walemavu wanakuwa katika wakati mgumu huku wengi wakiishi maisha yasiyo mazuri.
“Wengi wetu hasa wanaoishi maeneo ya vijijini hali yao kimaisha sio nzurio kwani wao wana matatizo,” alisema.

Akifungua mafunzo hayo, Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Noel Ndallu, alisema serikali inawathamini watu wenye ulemavu na ndiyo maana miundombinu inawekwa kwaajili yao ingawa jitihada bado hazitoshi.

Katika risala yao iliyosomwa na msaidizi wao, Focus Magwesela watu wenye ulemavu walisema wana mpango mkubwa katika kulitetea Taifa maendeleo kwa vile wana uwezo wa kufanya kazi.

Magwesela alisema pamoja na kuwa na ulemavu lakini wenye ulemavu wana haki ya kupata mahitaji ya msingi mfano elimu na mengineyo kama watu ambao hawana ulemavu.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanahudhuriwa na watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali yakiwa yameandaliwa na Chama cha Wasioona wilayani Urambo na kufadhiliwa na Foundation for Civil Society.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Walemavu Urambo walalamika kukosa elimu