Wazee wataka uwakilishi katika Bunge la Katiba

Wakati Muswada wa Pili wa Katiba Mpya ukitarajia kujadiliwa katika Bunge Maalum la Katiba mwezi ujao, wazee wa wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, wamekuja juu wakitaka kuwapo na uwakilishi wa wazee katika bunge hilo kama ilivyo kwa makundi ya vijana na walemavu.

Aidha, wameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupiga marufuku tabia iliyojengeka kwa shule za msingi hususani za vijijini walimu kuwapeleka wanafunzi mashambani huku wakiwa wamevaa sare za shule na kusababisha wazazi kuingia gharama za kufua nguo hizo.

Wazee hao wapatao 100 kutoka katika kata 10 za wilaya ya Mbarali, walitoa ombi hilo jana wakati wa semina kwa wazee kuhusu Sera ya Wazee ya mwaka 2005 iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Mbeya Hope for Orphans kwa ushirikiano na Mtandao wa Usangunet na kufadhiliwa na Shirika la Foundation for Civil Society.

Walilalamika kuwa serikali imewatenga wazee katika uwakilishi kwenye Bunge la Katiba hali itakayowanyima fursa ya kutetea maslahi ya kundi hilo ambalo ni kubwa katika jamii.

Walisema wana imani kuwa kama wazee wangekuwa na uwakilishi Bungeni hata suala la kutunga sheria kwa ajili ya Sera ya Taifa ya Wazee lingekuwa limeshapatiwa ufumbuzi kwani zaidi ya miaka 10 sasa sheria hiyo haijatungwa tangu ile ya awali ya mwaka 2003.

Aidha wazee hao, katika maazimio yao waliitaka serikali kuweka utaratibu wa kuwapatia pembejeo za kilimo wazee ili waweze kuongeza uzalishaji wa mazao na hivyo kuondokana na tatizo la uhaba wa chakula. Pia walilalamika kuwa pesheni wanayopata kwa mwezi ni ndogo mno, hivyo serikali ifikirie uwezekano wa kuiongeza angalau ifikie Sh.100,000 kwa mwezi na pia ichukue hatua kali kwa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwani vitendo hivyo vinailetea sifa mbaya Tanzania.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mbeya Hope for Orphans, Suzan Kisonga, alisema serikali iliona umuhimu wa kuwa na mwongozo wa kitaifa wa kuwa na Sera ya Wazee kama dira ya kuelekeza huduma kwa wazee.

Alisema Septemba 2003, Sera ya Taifa ya Wazee ilitolewa na serikali ikilenga hali ya wazee nchini, mmomonyoko wa maisha ya kijadi, matunzo duni, umaskini, magonjwa, wanawake wazee na mila zilizopitwa na wakati na sheria zisizolinda na kuendeleza wazee.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Gulam Hussein Kifu, aliipongeza asasi ya Mbeya Hope for Orphans kwa kutoa elimu kwa wazee juu ya haki zao zilizomo katika Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003.

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Wazee wataka uwakilishi katika Bunge la Katiba