Tarime walilia haki za wanaume

Wananchi wa Kata ya Mriba Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara wamesema katiba mpya ijayo itamke wazi haki za wanaume ili kuwalinda na unyanyasaji ambao unafanywa na wananwake kwenye ndoa.

Wakitoa maoni wananchi hao siku ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Chama cha Wakulima na Wafugaji (CHAWATA) walisema kuwa kuna haja katiba ijayo itamke wazi haki za wanaume asilimia 50 kwa 50 ili kuwalinda na unyanyasaji ambao unafanywa na wananwake wao wa ndoa.

 

Akizungumza Diwani mstaafu kata ya Mriba, Abdi Gasaya alisema kuwa baada ya wanawake kupewa haki wametumia nafasi hiyo vibaya na kuwanyanyasa wanaume ikiwa ni pamoja na kuwanyima tendo la ndoa kwa madai kuwa wamebakwa.

Mkazi wa Kijiji cha Mangucha,Philip Wambura akisema kuwa kutokana na wanawake kuwanyanyasa wanaume kuna haja katiba ijayo itamke wazi haki za wanaume na kuwalinda dhidi ya unyanyasaji uliopo kama vile kuwanyima chakula wakidai kuwa nenda ukale ulikokuwa.

Aidha, wananchi hao waliongeza kusema kuwa wanaunga mkono Tumeya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba kupendekeza Tanzania kuwa na Serikali 3 ambazo ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia walioongeza kusema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika zitajitegemea kiuchumi aidha uchumi utawezesha kila Serikali kustawi bila kutegemea serikali nyingine.

 

 

 

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Tarime walilia haki za wanaume