Viziwi waomba wakalimani

WALEMAVU wa kusikia kutoka Chama cha Michezo cha Viziwi mkoani Dodoma, wameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwahimiza wamiliki wa televisheni kuweka wakalimani ili nao wajue kinachoendelea duniani.

Walemavu hao walitoa kauli hiyo hivi karibuni kwenye mdahalo wa kujadili rasimu ya kwanza ya Katiba mpya uliofanyika mkoani Dodoma. Akizungumza na Tanzania Daima kwa niaba ya walemavu wenzake,

Kessy Yusuph, alisema mamlaka hiyo iamue kwa kila mmiliki atakayeshindwa kumuweka mkalimani kwa ajili ya viziwi wamfungie mitambo.

Yusuph ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi ya Viziwi iliyopo Kisasa mjini Dodoma, alisema wanapata shida, kwani katika sekta zote muhimu katika jamii inayowazunguka hakuna mkalimani.

“Sisi viziwi tumeachwa nyuma hata katika yale mambo ya msingi. Tumesahaulika bungeni, polisi, mahakamani, hospitali na hata katika vyombo vya habari

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Viziwi waomba wakalimani