Vunjo wataka Serikali moja katiba mpya

Wakazi wa Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, wamesema Serikali moja ya Muungano ndio suluhisho kwa watanzania na Muungano huo uliodumu kwa takriban miaka 50 sasa.

Wananchi hao walitoa mapendekezo hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya katiba mpya ulioandaliwa na taasisi ya he Foundation for Civil Society na kuendeshwa na taasisi inayoshughulika na haki za binadamu mkoani humo, KWIECO.

“Mfumo wa Serikali tatu utaurudisha nyuma nchi yetu kwa miaka 50 lakini tukiamua kuwa na serikali moja haya haya mambo saba tuliyooredheshewa hayatakuwa na sababu tena maana itakuwa nchi moja na serikali moja tu,”walisema wananchi hao katika mapendekezo yaliyowasilishwa na Immaculate Mworia.

Awali akitoa mchango wake katika kongamano hilo, mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Mwalimu Phares Mrema alisema kuwa rasmu hiyo imewekwa kama mtego kwa watanzania na kwamba wasipoijadili kwa makini watajikuta wanauvunja huo muungano wenyewe.

“ Ibara ndani ya rasimu hii inayopendekeza Serikali tatu pamoja na mambo saba ya kuzingatia ambayo yamewekwa mwisho kabisa ya rasimu hii ni mtego na ajenda iliyofichika ili kuwavuruga watanzania wakati wanaijadili katiba mpya na matokea yake Tanzania haitakuwepo tena”, alisema.

Aliongeza:’Kikubwa hapa ni iundwe serikali moja na baada ya hapa masuala yote yaliyowekwa kwenye rasimu hii yenye kulenga mrengo wa serikali tatu yaondolewe tupate katiba mpya, watanzani tuendelee kujenga nchi yetu,”Kwa upande wake, Hashim Mandari alipendekeza kuwa isistizwe ndani ya katiba hiyo mpya kuwa ardhi iendelee kuwa chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na unyeti wake.

“Tunaomba katiba mpya pia iainishe wazi kuwa wawekezaji wakija wapewe maeneo mapya watakayoyaendeleza wenyewe badala ya kupewa ardhi ambayo wananchi wazalendo washatengeneza na kasha wananchi hao wanahamishwa na kuachwa wakihangaika.”alisema.

 

 

 

Wasiliana Nasi

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Namba ya simu: +255 22 - 2664890-2
  • Nukushi: +255 22 - 2664893

Ungana na sisi

Tupo kwenye mitandao ya kijamii. Tufuate na uungane nasi.

Uko hapa: Home Chumba cha Habari Vunjo wataka Serikali moja katiba mpya