Shughuli za Kujengea na Kuendeleza Uwezo


Mbali ya kutoa ruzuku za aina mbalimbali, The Foundation for Civil Society pia inatekeleza shughuli mbalimbali za kujengea na kuendeleza uwezo wa asasi za jumuiya za kiraia. Shughuli hizi ni pamoja na utoaji wa mafunzo, Uimarishaji wa Ubia na Mitandao, Upashanaji wa Habari na Kujitangaza:

1. Utoaji wa Mafunzo –

Mafunzo ya aina mbalimbali yenye lengo la kuimarisha uwezo na kiutendaji wa jumuiya za kiraia huandaliwa na The Foundation kupitia wakufunzi maalumu. Mafunzo hayo hulenga kuimarisha uwezo wa jumuiya za kiraia katika maeneo yafuatayo; Uchambuzi wa Sera, Utunzaji wa Mahesabu ya Fedha, Uimarishaji wa Asasi (organisation development), na Ushawishi na Utetezi. The Foundation kwa kawaida huchambua mahitaji ya mafunzo kwa jumuiya za kiraia na kisha hutafuta wakufunzi wa kuyaandaa.

2. Mafunzo ya namna ya Kuendesha Miradi kwa Mashirika yanayopata Ruzuku kwa Mara ya kwanza – Baada ya kikundi au asasi kupata ruzuku, mafunzo ya siku tatu hutolewa. Lengo lake ni kuziwezesha asasi kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi na kwa matokeo yaliyotarajiwa. Mafunzo hayo hujumisha maeneo yafuatayo; hatua za mradi (project cycle), utunzaji wa vitabu vya mahesabu ya fedha (financial management) na namna ya kuandika ripoti za miradi na pia jinsi ya kufanya ufuatiliaji na tathmini yaani monitoring and evaluation.

3. Midahalo ya Wazi kuhusu Sera, Watu na Maendeleo (Ulingo wa Maendeleo) –

 

 

 

 

Hii ni midahalo inayoandaliwa kwa ustadi na kuwahusisha watu wa makundi mbalimbali katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini. Lengo lake kuu ni kuwawezesha wadau wote wa maendeleo kukutana, kujadili na kupanga mikakati ya pamoja kuhusiana na maendeleo katika mkoa au wilaya husika. Washiriki wa ulingo wa maendeleo ni pamoja na wawakilishi wa jumuiya za kiraia (wakulima, wawakilishi wa NGOs, wanawake, wanaume, watoto, na vijana), vile vile viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla. Tangu Novemba 2005, The Foundation inashirikiana na wadau wa mikoani kuandaa midahalo hii. Lengo lingine la midahalo ni kujenga uwezo wa asasi za kiraia katika kujihusisha na masuala ya ki-sera katika maeneo yao. Tangu Novemba 2005 midahalo kama hiyo imekwisha fanyika katika mikoa ya Mwanza kwa kushirikiana na MNGON, Morogoro kwa kushirikiana na UNGO, Rukwa kwa kushirikiana na RANGO, Kigoma kwa Kushirikiana na KIKANGONET na Dodoma kwa kushirikiana na MAMADO na NGONEDO. Pia katika Mikoa ya Musoma kwa kushirikiana na Foundation Help, Arusha kwa kuhsirikiana na ANGONET, Iringa kwa kushirikiana na ICISO, Zanzibar kwa pamoja na ANGOZA na Mtwara kwa kushirikiana na MANGONET na MRENGO. Masuala mbalimbali ya juu ya umasikini, utawala bora, afya, maji, mazingira, kilimo na demokrasia shirikishi yameibuliwa. Aidha baada ya midahalo jumuiya za kiraia huwa na makati maalumu wa utekelezaji na ufuatiliaji.

4. Utafiti – The Foundation huendesha utafiti wa aina mbalimbali kwa lengo la kubaini hali ya sekta ya jumuiya za kiraia, mafanikio na changamoto zake. Utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2000 kabla ya kuanzishwa kwa the Foundation. Matokeo yake yalibainisha umuhimu wa kuundwa kwa shirika hili ili kukidhi mahitaji ya kujengewa uwezo kwa jumuiza za kiraia.

5. Kuimarisha Ubia na Mitandao - Hili ni eneo jingine ambalo the Foundation inalitekeleza. Lengo ni kuziwezesha jumuiya za kiraia katika ngazi ya mikoa na wilaya ziweze kujifunza kutoka kwao wenyewe, kubadilishana uwezo na kutambua umuhimu wa kufanya kazi pamoja. Tangu Disemba 2005, The Foundation huandaa mikutano na mitandao kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na habari. Aidha hujadili namna ya kuwezesha huduma za The Foundation ziweze kufika katika maeneo ya mbali mikoani na wilayani.

6. Ufuatiliaji na Ushauri (monitoring and backstopping visits) – Tangu mwaka 2005, the Foundation inatekeleza filosofia ya “uwekezaji kwa mabadiliko” yaani “investor outcome approach”. Kwa mujibu wa mwelekeo huu, shirika linatekeleza shughuli zake kwa ukaribu na wadau wake. Lengo ni kuwezesha ubadilishanaji wa uzoefu, changamoto na mafanikio kwa ajili ya faida ya wote. Idara ya Ruzuku na Idara ya Maendeleo huandaa ziara mbalimbali kwa ajili ya kutathmini maendeleo na kutoa ushauri kwa wadau.

7. Utafutaji, Unadaaji na Usambazaji wa Habari – katika shughuli hizi, the Foundation hutafuta, kuandfaa na kusambaza habari kwa wadau wake. Habari hizi husambaza kupitia matamasha ya kila mwaka ya Jumuiya za Kiraia (CSO Annual Forums), Mikutano ya Upashanaji habari (information Sessions), na kupitia machapisho na tovuti. Lengo ni kuwawezesha wadau kujua mweleko wa shughuli zetu. Aidha the Foundation ina vituo mbalimbali mikoani kwa ajili ya kusambaza taarifa juu ya sera na maendeleo ya sekta ya jumuiya za kiraia.

Contact us

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Tel: +255 22 - 2664890-2
  • Fax: +255 22 - 2664893

Connect with us

We're on Social Networks. Follow us & get in touch.