WITO WA MAOMBI YA RUZUKU KWA ASASI ZA VIZIWI TANZANIA KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA LUGHA YA ALAMA MWAKA 2018

Desemba 15, 2017

1.     UTANGULIZI

Foundation for Civil Society (FCS) ni asasi huru iliyoanzishwa kama taasisi ya kimaendeleo isiyogawana faida, inayotoa ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa asasi za kiraia (AZAKI) nchini Tanzania. FCS ilisajiliwa na kutambulika rasmi kama chombo kilichopo kisheria mnamo Septemba ya 2002 na ikaanza shughuli zake rasmi mnamo Januari 2003.

FCS inafanya kazi katika kuhakikisha kwamba asasi za kiraia Tanzania zinakuwa chachu kwenye michakato ya maendeleo yenye kulenga kuleta mabadiliko kwa wananchi huku ikizingatia haki za makundi maalum katika jamii kama: Watu wenye Ulemavu, Wanawake, Watoto, Vijana na jamii zilizopo pembezoni.

 

Tangu kuanzishwa kwake FCS imekua ikifanya kazi ya kuyajengea uwezo na kutoa ruzuku mbalimbali kwa mashirika ya Watu wenye Ulemavu ili kuhakikisha wanapaza sauti zao katika kudai na kupata haki, uwakilishi katika ngazi mbalimbali na huduma bora kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Watu wenye Ulemavu (2010) na Mkataba wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu (UNCRPD) wa mwaka 2006.

2.     WITO WA MAOMBI YA RUZUKU KWA AZAKI ZA VIZIWI

Sheria ya Watu wenye Ulemavu (2010) sambamba na masuala mengine inatoa fursa ya kupata taarifa, kulindwa na kushiriki au kushirikishwa katika masuala ya kawaida ya kijamii kwa Watu wenye Ulemavu sawa na watu wengine katika jamii. Aidha, sheria hiyo inabainisha umuhimu wa kutoa huduma za kijamii kwa uwazi na kuheshimu utu na uhuru wa kila mtu wakiwemo Watu wenye Ulemavu. Kwa mujibu wa sheria hiyo, vyombo vya umma vinatakiwa kuzingatia utoaji wa Huduma za Jamii kwa Watu wenye Ulemavu bila kuwabagua au kuwatenga. 

Watu wenye Uziwi ni miongoni mwa makundi haya na wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za jamii. Kadhalika, Viziwi wanayo haki ya kusikilizwa ipasavyo na kupata haki kutoka katika vyombo vya ulinzi na maamuzi hapa nchini.  

Hata hivyo kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazozuia upatikanaji na ufikiwaji wa usawa katika huduma zinazotolewa na taasisi, vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vya maamuzi Tanzania. Miongoni mwa visababishi ni pamoja na mitazamo hasi kutoka kwa jamii kuhusu ulemavu na watu wenye ulemavu, kukosekana kwa miundombinu rafiki kwa Viziwi, kukosekana kwa wakalimani wenye ujuzi na uelewa duni wa Lugha ya Alama baina ya watendaji wa vyombo husika na Viziwi ambayo ni kiungo kikubwa cha mawasiliano baina ya Viziwi na watu wengine. 

Kwa kubaini changamoto hizo, FCS inakaribisha maombi ya ruzuku  kutoka katika Asasi za Kiraia za Viziwi na Vyama vya Viziwi, ambazo hazifungamani na Vyama vya Siasa, na hazitengenezi faida kutoka mikoa yote Tanzania kushiriki katika utekelezaji wa shughuli zinazolenga kuimarisha upatikanaji wa haki kwa viziwi kutoka katika vyombo vya ulinzi yaani Jeshi la Polisi, Magereza na Mahakama. 

3.     MALENGO NA MATOKEO TARAJIWA YA PROGRAMU HII. 

 

3.1 Malengo makuu ya kutekeleza programu hii ni: 

3.2 Matokeo yanayotarajiwa 

3.3 Shughuli zitakazofadhiliwa 

·       Shughuli zenye zenye tija na ubunifu wa namna makundi tajwa yatafikiwa ili kufanikisha malengo makuu ya wito huu. 

4.0 Kiwango cha ruzuku na Muda wa utekelezaji 

FCS itatoa kiwango kisichozidi shilingi milioni ishirini (20,000,000) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa miezi  minane (8). 

 

5.0 Vigezo vitakavyo zingatiwa katika kuidhinisha miradi

Kigezo kikuu kitakachozingatiwa katika kuidhinisha na kuuthibitisha mradi wowote ili kupata ruzuku kutoka FCS ni baada ya kujiridhisha kwamba shughuli za mradi husika zinadhihirisha pasipo shaka kuwa zitawanufaisha (moja kwa moja au kwa njia nyingine) walengwa wa maombi haya kama ilivyobainishwa katika Malengo Makuu ya wito huu.

Vigezo vingine mahsusi ambavyo vitazingatiwa katika uidhinishaji wa mradi ni;

a)    Ni kwa jinsi gani shughuli zilizopangwa katika andiko la mradi zinaendana na malengo makuu ya programu kama ilivyoelezwa kwenye tangazo.

b)    Ni kwa jinsi gani utekelezaji wa andiko mradi unaweza kupimika na kuchangia katika kupelekea ufanisi na urahisishaji wa upatikanaji wa huduma na utendaji wa vyombo vya maamuzi na vyombo vya usalama. 

c)    Uwezo na ubunifu wa miradi yenye kuleta tija kwa gharama nafuu.

d)    Nafasi ya jamii, kama vile, uwakilishwaji na ushirikishwaji, kiwango cha uhusishwaji wa jamii katika kuandaa, kuitambua na kutekeleza miradi inayowahusu.

e)    Kwa jinsi gani mradi utaweza kuinufaisha jamii hadi katika ngazi ya chini kabisa kwa uthibitisho wa takwimu na ushahidi.

f)      Uwepo wa nyaraka zote muhimu zinazohitajika katika fomu ya maombi, zikiwemo fomu ya bao mantiki, mpango kazi, na bajeti, zinazopatikana kwenye tovuti ya Foundation.

Kumbuka:  Orodha ya mambo yote muhimu imeambatanishwa katika fomu mpya ya maombi.

5.0 Taasisi zinazoalikwa kuleta maombi 

Taasisi na Asasi za viziwi na Vyama vya Viziwi tu na zenye vigezo vinavyohitajika, zinaweza kushiriki katika utekelezaji wa programu hii. Tafadhali jaza fomu inayopatikana katika tovuti ya FCS; www.thefoundation-tz.org

 

6.0  Shughuli na Asasi ZISIZOLENGWA kupata ruzuku kutoka FCS

 

FCS itatoa ruzuku kwa Taasisi ambazo zimesajiliwa kufanya shughuli ambazo hazizalishi faida. Kama maelezo na ufafanuzi zaidi vitahitajika juu ya kigezo hiki, basi wasiliana na FCS kabla haujafanya maombi yako ya ruzuku.

FCS haitatoa ruzuku kwa:

·       Udhamini na ufadhili

·       Miradi au shughuli zitakazo fanyika nje ya Tanzania

·       Miradi au shughuli ambazo zimeshawahi kufanyika na kukamilika.

·       Miradi ambayo imekwisha wezeshwa ruzuku na mashirika mengine.

·       Kutumika kama Malipo ya ziada kwa wafanyakazi wanaolipwa na taasisi husika

·       Kipato cha mtaji kwa taasisi ndogondogo za fedha

·       Maombi toka kwa wataalamu wa ushauri au watunisha mifuko kwa niaba ya taasisi.

·       Watu binafsi

·       Vyama vya siasa

·       Miradi ambayo inalenga kuinufaisha dini/dhehebu Fulani, kabila Fulani au kikundi Fulani chenye mlengo wa kikabila.

·       Sekta binafsi (isipokuwa kama haipo kwa ajili ya manufaa ya kuzalisha faida)

·       Taasisi zenye madeni

·       Waendesha Semina, warsha, na mikutano  tu, isipokuwa kama ni sehemu ya shughuli zilizounganishwa na tokeo mahususi.

·       Gharama kubwa zisizo tarajiwa (dharura)

·       Utoaji wa huduma za jamii

·       Maombi ya mkakati wa ruzuku katika utekelezaji wa miradi ya UKIMWI

 

ANGALIZO KWA WAOMBAJI WOTE

 

Foundation for Civil Society, ni asasi ya kiraia inayojitegemea kimamlaka. Tunayo sera ya  kuendesha shughuli zetu zote kwa uaminifu, kimaadili na uwazi. Katu hatuvumilii hongo na rushwa, kwani tumejitoa kuendesha mambo yetu kitaalamu, kwa haki, na uadilifu katika shughuli zetu na mahusiano yote. Kwa hiyo tunawasihi waombaji wote kufuata utaratibu uliowekwa wa kupata ruzuku kutoka FCS, kwa kutumia daima njia sahihi za mawasiliano. Ili kuwasiliana nasi, piga simu kupitia nambari+255 22 266 4890-2, simu ya mkononi  +255 754 005708 au barua pepe:  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. .  

 

7.0  Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi 

 

Maombi yote yaliyofanyiwa tafakari ya kina na mapendekezo ya miradi yaliyoandikwa vyema yanatakiwa yatumwe na kumfikia Mkurugenzi Mtendaji kabla ya saa 10.00 jioni mnamo tarehe 22 Januari, 2018. Maandiko ya miradi yatakayotumwa baada ya tarehe ya mwisho ya kutuma maombi hayatafikiriwa kwa ajili ya kupewa ruzuku na FCS.

8.0  Jinsi ya kutuma maombi

 

Andiko la mradi lililokamilika linatakiwa kuwasilishwa kwa nakala halisi (Hard Copy na  siyo kwa njia ya kielektroniki au kwa barua pepe). Kwa mantiki hiyo fomu zote zilizojazwa vizuri zinatakiwa kutumwa kupitia sanduku la barua/posta kwa anuani ifuatayo:

 

Kwa Mkurugenzi Mtendaji

Foundation for Civil Society

7 Madai Crescent, Ada Estate Plot Na. 154

S.L.B 7192

Dar es Salaam 

 

Simu ya mezani          +255 22 266 4890-2

Simu ya mkononi        +255 754 005708

 

Tovuti: www.thefoundation.or.tz