Kongamano la AZAKI lataka Utangamano wa Afrika Mashariki ulio imara, unaotokana na wananchi

Kongamano la Asasi za Kiraia Tanzania juu ya Utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni limeafiki wito wa kuwa na utangamano wa Afrika Mashariki imara na sio legelege, unaotokana na unaoongozwa na wananchi wenyewe.

Ikiwa ni sehemu ya hitimisho la kongamano la siku mbili la wana AZAKI liliandaliwa na Foundation for Civil Society (FCS) na kumalizika Novemba 27 mwaka huu, washiriki walikubaliana kwa ujumla wao na kuzitaka nchi wanachama kuhakikisha Jumuiya inakuwa na utangamano imara ambao utatokana na kuongozwa na wananchi ili kuleta maendeleo endelevu.

Kongamano hilo la AZAKI pia lilifikia maazimio yake juu ya nafasi ya Tanzania katika kufanikisha utangamano wa Afrika ya Mashariki ambao wanautaka. Kwa makubaliano ya pamoja pia, washiriki kutoka Asasi za Kiraia wameitaka nchi ya Tanzania kuwa kinara na mstari wa mbele katika kuhakikisha utangamano imara wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, unaotokana na kuongozwa na wananchi wenyewe unafanikiwa.

“Hata kama tukirudi nyuma na kuangalia historia, Tanzania ndio ilikuwa kinara katika ukanda huu iliyochukua uongozi madhubuti wa kufanikisha uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo kwa bahati mbaya ilivunjika mwaka 1977. Kwa hiyo hakuna haja ya Tanzania kusita kuichukua nafasi yake tena kama kinara wa kuhakikisha utangamano imara wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki unapatikana,” alisema mmoja ya watoa mada katika kongamano hilo, Dk. Kitila Mkumbo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Pia mhadhiri mwingine, Dk Azaveli Lwaitama, ambaye pia alitoa mada katika kongamano hilo alisema: “Endapo tunahitaji kuwa na utangamano imara, tunahitaji kufikiwa mapema kwa hatua ya Ushirikiano wa Kisiasa ili uweze kuwa chachu ya kudhibiti hatua nyingine zote muhimu za utangamano imara, kama vile Umoja wa Ushuru, Soko la Pamoja na uwepo wa Sarafu Moja.”

“Sisi kama Asasi za Kiraia, wajibu wetu mkuu ni kuwa vinara wa hufanikisha mijadala na utoaji wa elimu katika jamii zetu ili kuwa na utangamano imara, unaotokana na kuongozwa na wananchi wenyewe,” alisema Bw. John Ulanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society.

 Kongamano hilo la AZAKI ilikutanisha washiriki takribani 130 (30 kutoka nchi nyingine wananchama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki) huku mada kuu ikiwa ni: “Wajibu wa Asasi za Kiraia katika kuimarisha utangamano wa Afrika ya Mashariki.”

Viziwi waomba wakalimani

WALEMAVU wa kusikia kutoka Chama cha Michezo cha Viziwi mkoani Dodoma, wameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwahimiza wamiliki wa televisheni kuweka wakalimani ili nao wajue kinachoendelea duniani.

Walemavu hao walitoa kauli hiyo hivi karibuni kwenye mdahalo wa kujadili rasimu ya kwanza ya Katiba mpya uliofanyika mkoani Dodoma. Akizungumza na Tanzania Daima kwa niaba ya walemavu wenzake,

Read more: Viziwi waomba wakalimani

Vunjo wataka Serikali moja katiba mpya

Wakazi wa Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, wamesema Serikali moja ya Muungano ndio suluhisho kwa watanzania na Muungano huo uliodumu kwa takriban miaka 50 sasa.

Wananchi hao walitoa mapendekezo hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya katiba mpya ulioandaliwa na taasisi ya he Foundation for Civil Society na kuendeshwa na taasisi inayoshughulika na haki za binadamu mkoani humo, KWIECO.

Read more: Vunjo wataka Serikali moja katiba mpya

Tarime walilia haki za wanaume

Wananchi wa Kata ya Mriba Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara wamesema katiba mpya ijayo itamke wazi haki za wanaume ili kuwalinda na unyanyasaji ambao unafanywa na wananwake kwenye ndoa.

Wakitoa maoni wananchi hao siku ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Chama cha Wakulima na Wafugaji (CHAWATA) walisema kuwa kuna haja katiba ijayo itamke wazi haki za wanaume asilimia 50 kwa 50 ili kuwalinda na unyanyasaji ambao unafanywa na wananwake wao wa ndoa.

Read more: Tarime walilia haki za wanaume

Contact us

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Tel: +255 22 - 2664890-2
  • Fax: +255 22 - 2664893

Connect with us

We're on Social Networks. Follow us & get in touch.
 

     

You are here: Home News Room Habari & Matukio