Historia

The Foundation for Civil Society ilisajiliwa Septemba 2002 na ilianza shughuli zake rasmi Januari, 2003 kama kampuni isiyozalisha faida iliyobuniwa na kupata ufadhili kikundi cha wabia wa maendeleo waliokuwa na azma ya pamoja, ni shirika lilio chini ya utawala wa bodi huru.


The Foundation inawezesha wananchi kuwa na msukumo ulio imara wa kuleta mabadiliko katika kuboresha utawala wa kidemokrasia nchini Tqanzania, katika kupambana na umasikni na kuleta maisha yaliyo bora kwa wote.
Foundation imekua kutoka wazo mpaka taasisi kubwa. Namba ya ruzuku zinazotolewa imeongezeka kutoka 36 mwaka 2003 mpaka kufikia jumla ya ruzuku 621 zinazoidhinishwa kila mwaka.


Kiwango na ukubwa wa Ruzuku pia umeongezeka. Mwaka 2003 kulikua na jumla ya miradi 53 inayofadhiliwa yenye thamani ya shilingi 807,210,000 lakini mpaka kufikia mwisho wa mwaka 2012 jumla ya miradi 890 yenye thamani ya shilingi 17,573,806,000 ilifadhiliwa.


Huduma zetu zimetanuka katika mikoa 30 mwaka 2013 kutoka mikoa 14 mwaka 2003.
Zaidi ya asilimia 60 ya miradi inayofadhiliwa na Foundation inatekelezwa Vijini, mwaka 2003 asilimia 15 pekee ndio ilikuwa miradi iliyolenga maeneo ya pembezoni.


Bajeti ya jumla imeongezeka kutoka dola za kimarekani milioni 2.5 mwaka 2003 hadi kufikia dola za kimarekani milioni, vilevile tangu mwaka 2003, Foundation imepokea jumla ya dola za kimarekani 67,631,497 kutoka kwa wafadhili.
Matumizi yetu kwa mwaka yameongezeka, kutoka matumizi ya Dola za kimarekani milioni 1.8 mwaka 2003 hadi million 13 mwaka 2012.


 Wafadhili wetu wameongezeka kutoka 3 mwaka 2003 mppaka kufikia idadi ya wafadhili 8 mwaka 2012. Wafanyakazi ia wameongezeka kutoka 21 mwaka 2003 hadi kufikia 31 mwaka2016.

Contact us

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

  • Tel: +255 22 - 2664890-2
  • Fax: +255 22 - 2664893

Connect with us

We're on Social Networks. Follow us & get in touch.