Let us know below
NEWSButiama wataka katiba Vijijini
2012
JUNE
18th
Wananchi wa Kata ya Kukilango katika Wilaya mpya ya Butiama, mkoani Mara wameitaka serikali kusambaza katiba vijijini ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa kabla ya kutoa maoni yao kwenye tume ya katiba.Wananchi hao walitoa kauli hiyo hivi karibuni kwa nyakati tofauti kwenye mdahalo wa kupata maoni juu ya uundwaji wa katiba mpya ulioandaliwa na mtandao wa asasi za kiraia mkoa wa Mara (Mara Forum) chini ya ufadhili wa the Foundation for civil society. Walisema pamoja na serikali kuunda tume hiyo, wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini hawajapata elimu ya kutosha kuhusu zoezi la kutoa maoni pamoja na kutoifahamu katiba iliyopo. Akichangia mada katika mdahalo huo, mkazi wa kijiji cha Kiabakali, Verena Charles, alisema wananchi wengi hawajui katiba na wala hawajawahi kuiona, hivyo itakuwa ni vigumu kwao kutoa maoni kwenye tume hiyo. Naye John Nyamsana, alisema wananchi wanahitaji katiba mpya itakayokidhi mahitaji na matakwa yao tofauti na sasa ambapo katiba ipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu wachache. Wawezeshaji katika mdahalo huo, Bonmatto kutoka Asasi ya Shehabita Tarime na Mwanasheria Paschal Patroba walitumia fursa hiyo kuwafafanulia wananchi mambo mbali mbali kuhusu katiba iliyopo na kujitokeza kwa wingi wakati wa kutoa maoni. Chanzo: Tanzania Daima, 15/6/2012 |
