Download
Useful Links
cso websites funded by fcs
Your Comments
Do you have questions/comments?
Let us know below
Let us know below
| FCS Forum | Login | Feedback |
TOPIC
13/07/2010
MAFUNZO YA KUJENGA UZOEFU WA KAZI KWA WANAFUNZI, NI NJIA SAHIHI YA KUMUANDAA KIJANA KUWAJIBIKA VIZURI MAENEO YA KAZI?
Asasi na mashirika mbalimbali yamekuwa yakishauriwa kuwachukua wanafunzi wa vyuo vikuu wanapokuwa kwenye mafunzo ya vitendo mara kwa mara. Nia kuu imekuwa kumuwezesha kijana kupata uzoefu wa kazi na kumtayarisha kukabiliana na changamoto za maisha. Je kwa mtazamo wako ni kweli hili limekuwa likifanyika kwa ufasaha na ni kwa kiasi gani vijana wamenufaika na utaratibu huu?
Asasi na mashirika mbalimbali yamekuwa yakishauriwa kuwachukua wanafunzi wa vyuo vikuu wanapokuwa kwenye mafunzo ya vitendo mara kwa mara. Nia kuu imekuwa kumuwezesha kijana kupata uzoefu wa kazi na kumtayarisha kukabiliana na changamoto za maisha. Je kwa mtazamo wako ni kweli hili limekuwa likifanyika kwa ufasaha na ni kwa kiasi gani vijana wamenufaika na utaratibu huu?
RAJAB KABAVAKO
25/08/2010
Mimi ninaamini kuwa mafunzo ya kujenga uzoefu wa kazi kwa wanafunzi ni mazuri na ni njia sahihi ya kumuandaa kijana kuwajibika vizuri katika maeneo yake ya kazi. kwani iwapo atakutana na wachapa kazi akafanya nao kazi, atawaiga uchapaji kazi wao lakini bahati mbaya kama akikutana na watu wavivu na wachoyo anaweza kutoka bila kujua kitu, hapa tatizo si mfumo bali watu waliomuandaa ndio wabaya.
WISE
13/07/2010
Hi,
Ushauri wangu ni kuwa ni kitu kizuri kuwapa fursa watanzania wenzetu vijana kupata uzoefu. Tatizo soko wameliaribu wenyewe mara nyingi hawana utulivu na umakini wa kazi wanafikiri fursa wanazopewa ni mahali pa kufanya mchezo mchezo vi excuse vya kutohudhuria mara kwa mara na wakati mwingine hawaji. Kwa ufupi nidhamu ni shida.
Ni vema anayewachukua aliweke wazi hilo. Pia hata chuo chenyewe kupitia waalimu wanaowasimamia ni tatizo. Hata wakipewa mrejeso juu ya mapungufu ya wananfunzi wao hawalifanyii kazi tatizo hilo na nilichogundua PT aiwei attached kwnye maksi za wanafunzi japo wanataka CSO ijaze form fulani. Na kama vile haitoshi pamoja na kuwapa angalizo kwa maandishi na kutojibu, mwaka unaofuata kama vile hawajui au wanadhani umesahau wanakuja tena na barua ya kuomba fursa tena na walimu wale wale wasiokuja kuwapitia wala kufanyia kazi changamoto.
Mimi bado nadhani kama mzalendo ni fursa nzuri lakini ili msije shangaa mwisho wa siku kuwa kero badala ya faida ni vema kuwepo makubaliano na idara husika kuhsu ufuatiliaji, kusughulikia changamotona pia wanafunzi kupewa code of conduct na hasiye abide afukuzwe kwani kila upande unahitaji mwenzie na hivyo dhana ya kuwa anayefaidika ni asasi isiwepo.
Ila nataka kusifi idara ambazo kwao mpaka wana ofisi inayoshughulikia placement za wanfunzi-engeneering-hsipoenda ulikopangiwa na husipohudhuria hawakusemeshi utakuta katika matoke yako anscond ata kama ni mwaka wa nne kumbe mwalimu alipoenda pale hakukukuta na alipewa taarifa hakuseshi anakupa maksi unazostahili utajiju ukijikuta ume disco mwisho wa siku.
Ila pia nasi wana CSO. Kuna baadhi yetu wanacukua hawa vijana hakuna job description anakuja fanya nini hakuna hata on job training ya kazi iliyomleta mtu akiamka asubui leo anamtuma hiki kesho kile kaa kibarua mwisho wa kukaa hapo hawezi sema nilijifunza nini. Nadhani kama tunapenda kuwaheshimu wenzetu pamoja na ujuzi wao kidogo tuwatendee haki kwa kujiandaa na kuwaandalia cha kufanya na kuwapa fursa ya kujifunza kazi si kutumwa tumwa kusikomjenga mtu kitaaluma na kikazi
Kwa nia njema fursa hii tuichangamkie kwa kuweka mazingira mazuri kila upande unufaike
Recent Topics
| Title | Views | Last Updated |
| NINI MTIZAMO WAKO KUHUSU BIASHARA NA SIASA? | 0 | 26/08/2010 |
| NINI KINAFUATA ZANZIBAR? | 0 | 12/08/2010 |
| Asasi za kiraia zina mchango gani katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu? | 0 | 12/08/2010 |
| MAFUNZO YA KUJENGA UZOEFU WA KAZI KWA WANAFUNZI, NI NJIA SAHIHI YA KUMUANDAA KIJANA KUWAJIBIKA VIZURI MAENEO YA KAZI? | 0 | 13/07/2010 |
| WHAT HAS BEEN THE ROLE OF CIVIL SOCIETY AFTER INDEPENDENCE IN AFRICA? | 0 | 13/07/2010 |
Top Contributors
| Lina [ 1 ] |
| Kelvin [ 2 ] |
| Noel [ 1 ] |
| James [ 1 ] |
| Hermengild Mayunga [ 2 ] |
| Michael Mpombo, KILI CENTRE, MOSHI. [ 1 ] |
