Home | Vacancies | Join our mailing list | Webmail | CSO Directory | FCS Forum       ENGLISH‹›SWAHILI
..enabling effective engagement in poverty reduction efforts!
What they Say About Us
  • About Us
  • Grants
  • Services
  • Reports & Plans
  • publications
  • contact us
   
 
Download
  • The Foundation News Civil Society’s Role During...
  • Keystone’s East African Grantee Feedback Report 20...
  • Audited Accounts 2009
  • New Application Form
  • New Application Guide
  • More »
    Useful Links
  • National civil society networks and organizations
  • Regional and global civil society networks
  • Others
  • CSO Directory
  • cso websites funded by fcs
  • Ruvuma Orphans Association
  • paralegal
  • Christian Council Of Tanzania
  • Guluka Kwalala
  • More »
    Your Comments
    Do you have questions/comments?
    Let us know below

    Name
    E-mail
    Comment
     
    FCS Forum Login Feedback
    Recent Topics
    Title Views Last Updated
    NINI MTIZAMO WAKO KUHUSU BIASHARA NA SIASA? 0 26/08/2010
    NINI KINAFUATA ZANZIBAR? 0 12/08/2010
    Asasi za kiraia zina mchango gani katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu? 0 12/08/2010
    MAFUNZO YA KUJENGA UZOEFU WA KAZI KWA WANAFUNZI, NI NJIA SAHIHI YA KUMUANDAA KIJANA KUWAJIBIKA VIZURI MAENEO YA KAZI? 0 13/07/2010
    WHAT HAS BEEN THE ROLE OF CIVIL SOCIETY AFTER INDEPENDENCE IN AFRICA? 0 13/07/2010
    Top Contributors
    Lina   [ 1 ]
    Kelvin   [ 2 ]
    Noel   [ 1 ]
    James   [ 1 ]
    Hermengild Mayunga   [ 2 ]
    Michael Mpombo, KILI CENTRE, MOSHI.   [ 1 ]
    Recent Comments
    Comment User name Posted On
    Nionavyo mimi ni kuwa mabadiriko yanayotokea Zanzibar ni matokea ya Sera za Mheshimiwa Rais Kikwete kwani tokea awali aliazimia kuondoa mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Hivyo matokea ya Kura ya maoni ya Zanzibar ni kuleta usalama na amani kwa Wazanzibar wote na uchaguzi wa safari hii tunategemea utakuwa huru na wa haki vinginevyo kutakuwa na unafiki ndani yake. RAJAB KABAVAKO 25/08/2010
    Jukumu la AZAKI katika kipindi hiki cha uchaguzi ni kama ifuatavyo: 1. kutokupendelea chama chochote cha siasa kwani vinginevyo zitapoteza uelekea na kusababisha vurugu. 2. kutoa elimu ya uraia na upigaji kura kwa Watanzania. Kwamba kila mtu lazima achague kiongozi amtakaye 3. kuwa waangalizi wa ndani wa uchaguzi na kuwa tayari kusema ukweli kwa kila kinachotokea katika kipindi hiki cha uchaguzi bila kufumbia macho maovu hata kama yatafanywa na chama tawala. RAJAB KABAVAKO 25/08/2010
    Mimi ninaamini kuwa mafunzo ya kujenga uzoefu wa kazi kwa wanafunzi ni mazuri na ni njia sahihi ya kumuandaa kijana kuwajibika vizuri katika maeneo yake ya kazi. kwani iwapo atakutana na wachapa kazi akafanya nao kazi, atawaiga uchapaji kazi wao lakini bahati mbaya kama akikutana na watu wavivu na wachoyo anaweza kutoka bila kujua kitu, hapa tatizo si mfumo bali watu waliomuandaa ndio wabaya. RAJAB KABAVAKO 25/08/2010
    Yanayotokea Zanzibar kwa sasa ni mema sana na kwa manufaa ya kisiasa na utulivu wa nchi. Hata hivyo, mchakato wa kura ya maoni ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, nayaona yanaenda kinyume na Utawala wa Sheria. Nasema hivi kwa kuwa, kuna mambo ya msingi ambayo nadhani yangepaswa kujadiliwa na Muungano, kwani tunajua fika kuwa Zanzibar si dola, japo mabadiliko hayo yameifaya/kuitamka kuwa ni dola (nchi huru). Shirika langu linakusudia (siku za usoni) kuandaa mjadala mkubwa wa wazi juu wa hali ya kisiasa ya Zanzibar kwa sasa kufuatia mabadiliko haya makubwa. Rodrick Maro 20/08/2010
    Kwa maoni yangu AZAKI nyingi zimekuwa kimya sana kwa zile zilizojaribu kutoa mwelekeo hazikufanya kwa kina na kwa mwelekeo uliopasika. Kuna mambo mengi yamejitokeza kuelekea uchaguzi mkuu yanayopingana na maadili ya Democrasia Asasi nyingi zimekuwa kimya. Rushwa ukiukwaji wa haki za kupata viongozi wenye maadili zimekuwa kimya kukemea kwa uwazi. kuonyesha mwelekeo angalao wa kuwapa wananchi wa kawaida kujua kiongozi anayetakiwa ni yupi. Zimekuwa kimya. Wataalamu wa Kikatoliki walipotoa Nyaraka mbalimbali za kutoa mwelekeo wa angalao ni kiongozi gani Tanzania tunamtaka na Serikali na viongozi wa siasa walikemea sana ASASI zilikaa kimya chache sana zilijitokeza angalao kuunga mkono na nyingine kupinga. zilizopinga hazikutoa mbadala wake. kwa maoni yangu Asasi za kiraia zinatakiwa ziamke na kuonyesha mwelekeo. Tuamke tuseme hawa hawatufai na tutoe sababu za kutofaa kwao na nini tunataka kwa maslahi ya Tanzania. Fortunatus Fungatwende 19/08/2010
    Hi, Ushauri wangu ni kuwa ni kitu kizuri kuwapa fursa watanzania wenzetu vijana kupata uzoefu. Tatizo soko wameliaribu wenyewe mara nyingi hawana utulivu na umakini wa kazi wanafikiri fursa wanazopewa ni mahali pa kufanya mchezo mchezo vi excuse vya kutohudhuria mara kwa mara na wakati mwingine hawaji. Kwa ufupi nidhamu ni shida. Ni vema anayewachukua aliweke wazi hilo. Pia hata chuo chenyewe kupitia waalimu wanaowasimamia ni tatizo. Hata wakipewa mrejeso juu ya mapungufu ya wananfunzi wao hawalifanyii kazi tatizo hilo na nilichogundua PT aiwei attached kwnye maksi za wanafunzi japo wanataka CSO ijaze form fulani. Na kama vile haitoshi pamoja na kuwapa angalizo kwa maandishi na kutojibu, mwaka unaofuata kama vile hawajui au wanadhani umesahau wanakuja tena na barua ya kuomba fursa tena na walimu wale wale wasiokuja kuwapitia wala kufanyia kazi changamoto. Mimi bado nadhani kama mzalendo ni fursa nzuri lakini ili msije shangaa mwisho wa siku kuwa kero badala ya faida ni vema kuwepo makubaliano na idara husika kuhsu ufuatiliaji, kusughulikia changamotona pia wanafunzi kupewa code of conduct na hasiye abide afukuzwe kwani kila upande unahitaji mwenzie na hivyo dhana ya kuwa anayefaidika ni asasi isiwepo. Ila nataka kusifi idara ambazo kwao mpaka wana ofisi inayoshughulikia placement za wanfunzi-engeneering-hsipoenda ulikopangiwa na husipohudhuria hawakusemeshi utakuta katika matoke yako anscond ata kama ni mwaka wa nne kumbe mwalimu alipoenda pale hakukukuta na alipewa taarifa hakuseshi anakupa maksi unazostahili utajiju ukijikuta ume disco mwisho wa siku. Ila pia nasi wana CSO. Kuna baadhi yetu wanacukua hawa vijana hakuna job description anakuja fanya nini hakuna hata on job training ya kazi iliyomleta mtu akiamka asubui leo anamtuma hiki kesho kile kaa kibarua mwisho wa kukaa hapo hawezi sema nilijifunza nini. Nadhani kama tunapenda kuwaheshimu wenzetu pamoja na ujuzi wao kidogo tuwatendee haki kwa kujiandaa na kuwaandalia cha kufanya na kuwapa fursa ya kujifunza kazi si kutumwa tumwa kusikomjenga mtu kitaaluma na kikazi Kwa nia njema fursa hii tuichangamkie kwa kuweka mazingira mazuri kila upande unufaike WISE 13/07/2010
    Sisi Wafanyakazi wa ASIZE (NGOs) za Kitaifa na Kimataifa tunahitaji kuwa na umoja wetu wa wafanyakazi kwa sababu kuu moja. Ukijaribu kuangalia vyama vilivyo vingi vya wafanyakazi vinaundwa na wanachama walio wengi na wanaotoka katika mashirika mengi amabyo ni ya kifaida zaidi kwa mfano viwanda, makampuni ya uchimbaji madini, mafunta, makampuni ya utalii, kilimo, uvuvi, ufugaji, n.k. Sisi kaka ASIZE (NGO's), sifa zetu kubwa na kuu ni kwamba sisi sio mashirika ya kiserikali, sio mashirika ya kutengeneza faida za kifedha, sio mashirka ya kidini, sio mashirika ya kisiasa, nk. hivyo ni vyema kuwa na chombo chetu kitakachofanania na sifa hizi ili kiweze kujali maslahi yetu kwa kuzingatia misingi. ASIZE zilizo nyingi zimesajiliwa na zian wafanyakazi ambao hulipa kodi kwa serikali (PAYE), hivyo hata kama tutkakjuwa chini ya TUCTA ingekuwa ni jambo la busara kuwa na chombo chetu kwanza ambacho kingeweza kufanya uwakilishi wa kiusahaihi katika chombo chochote cha kutetea haki za wafanyakazi kilichopo ngazi ya taifa na kimataifa. Naunga mkono hoja ya kuwanzishwa kwa umoja wa wafanyakazi wa ASIZE. Michael Mpombo, Moshi. Michael Mpombo, Moshi 12/05/2010
    Jukumu la kulea watoto yatima wa Tanzania ni la watanzania wote kwa ujumla kimsingi. Jambo hili kwasasa limebaki tu kinadharia maana kivitendo jukumu hili limeachiwa kwa asasi za kiraia ambazo misaada yake mingi huipata si kutoka kwa watanzania wenyewe bali kwa wageni wanaotoka inje ya Tanzania.Ndugu, jamaa, marafiki na jamii ya kitanzania ya watoto yatima kwa hivi sasa imebaki na mtizamo kuwa jukumu hili si lao tena bali ni la mashirika ya kuhudumia watoto yatima ambapo kiukweli jamii ya kitanzania inachangia kwa kiasi kidogo sana katika malezi ya watoto hawa hata wawapo kwenye vituo vya watoto yatima. Huu ni mtizamo wa jamii yetu ambao haujengi hata kidogo juu ya muafaka wa nani anawajibika na tatizo hili. Jukumu hili ni letu wote sisi watanzania. Tunajitia aibu kwa kuendelea kutegema misaada toka wageni katika malezi ya watoto yatima. Jamii yote kwa ujumla kuanzia ngazi ya familia, ukoo, kitongoji, kijiji/mtaa, kata, tarafa, wilaya, mkoa na taifa inawajibika na jambo hili moja kwa moja. Lakini je tunalifahamu hilo na tupo tayari kuwajibika na hilo!Hata tukiwa tayari na uwajibikaji, je ni kwa kiwango gani!Serikali moja kwa moja inawajibika na suala hili kwani kila raia wa inchi hii ana haki sawa na mwingine na anapaswa kupata fursa sawa na mwingine. Kwa watoto yatima ambao tunategemea baadae ndio watakaokuwa wazalishaji wazuri na kulipatia taifa pato la kutosha, serikali inpaswa kuwasaidia pindi wanapokuwa hawana mtu wa kuwasaidia. Kimsingi kila mzazi anawajibika na mtoto wake, kwa watoto yatima ni kwamba wazazi wao wote wamekufa au mzazi mmoja amekufa, hivyo watoto hawa hawana ungalizi wa kutosha na kuendelezwa. Naomba, serikali ikishirikiana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa watoto yatima kuwajibika na hili. Ninapotamka serikali siamanishi serikali kuu tuu, ni serikali kuanzia ngazi ya kitongoji, mtaa, kijiji, kata, n.k Ninaamini kuwa taifa lolote hapa duniani, haliwezi kuendelea vizuri kama litarithiwa na raia wake ambao hawana ujuzi na uelewa/ufahamu wowote katika kukabiliana na changamoto zozote za kiuchumi. kisiasa, kijamii, n.k. Kama tunataka taifa letu lizidi kuendelea tunahitaji kuwekeza kwa watoto wetu maana ndio watakaokuwa wakala wa maendeleo ya taifa letu. Yatima ni miongoni mwa watoto ambao nao wanahitaji kulirithi taifa lao ili wazidi kuliendeleza kwa manufaa ya jamii yote kwa ujumla. Nasema jukumu la kulea watoto yatima wa Tanzania ni letu sisi watanzania, tukianzia ngazi ya familia, ukoo, kitongoji na hadi ngazi ya taifa. Tubadilike, tutumie rasilimali tulizonazo kufanya chochote tuwezacho kuhakikisha watoto hawa wanasaidika. Asante,Michael Mpombo, Kili Centre. Michael Mpombo, KILI CENTRE, MOSHI. 05/05/2010
    Ni kweli asasi zetu za kiraia zinashindwa kujiendesha kwa sababu zinategema mno ruzuku kwa asilimia mia moja na ruzuku hizi zilizo nyingi hazitoki Tanzania bali zinatoka kwa wahsani mbalimbali waliopo inje ya inchi. Wahsani hawa wanaotupatia sisi ruzuku ili kuendesha shughuli zetu za asasi mabalimbali za kiraia na kwaajili ya kuleta maendeleo chanya kwa watanzania wenzetu, huwa na malengo yao binafsi ambayo kwa watu wa kawaida tu hawawezi kugundua kuwa yanaendeleza kukua kwa umaskini wetu. Ruzuku wanazotupatia wahsani hawa ukiangalia mara nyingi hulenga maslahi yao zaidi kuliko maslahi ya walengwa katika mradi wa aina yoyote. Sikatai kuwa wapo wachache (wahsani) ambao huwa ni washirika wa kweli katika kuleta maendeleo yetu lakini walio wengi hutusaidia ili tuendelee kuwa maskini na wazidi kututawala kifikra,kiuchumi, kisiasa, kijamii, n.k. Asasi za kiraia hapa Tanzania zilizo nyingi haziwezi kupunguza umaskini wa watanzania kwa sababu zenyewe hazina mikakati mathubuti ya kuanzisha miradi ambayo itawaingizia vipato ambavyo watavitumia katika tutekeleza shughuli zao za maendeleo kwa raia. Ruzuku tupewazo na wahsani zina masharti lukuki ambayo kwa namna moja au nyingine ni unyanyasaji wa kifikra kwa sababu ili upate ruzuku ya kwao ni laazima uimbe wimbo wao na uzungumze lugha yao pasipo kujali kuwa na sisi tuna wimbo wetu na lugha yetu. Ili tuweze kuimba wimbo wetu na kuzungumza lugha yetu ni laazima tuwe na mikakati ya maksudi ya kuwa na vianzo vyetu vya ndani vya kujipatia ruzuku. Ni vizuri kwa serikali kutenga budget kwaajili ya kuzisaidia asasi za kiraia kutekeleza majukumu yake maana kila litekelezwalo na asasi yoyote ya kiraia ilipaswa kutekelewa na serikali, hivyo si mbaya kwa serikali kufanya asasi kuwa wakala wake wa kutekeleza baadhi ya shughuli ambazo ilipaswa kuzitekeleza. Vile vile tuwe na miradi ya kuzalisha sisi kama asasi za kiraia ili tusitegemee kwa asilimia mia moja kutekeleza shughuli zetu kwa kupitia ruzuku za wahsani, Asante, Michael Mpombo, Kili Centre. Michael Mpombo, Kili Centre, Moshi. 05/05/2010
    Mji wetu wa Moshi katika suala la KERO YA UCHAFU NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA kweli upo makini na suala hili. Maana wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuweka miundo mbinu amabayo inapunguza uchafu na uchafuzi wa mazingira. Mji huu vile vile umeweka sheria, taratibu na adhabu kwa yoyote atakayebainika kufanya uchafuzi wa mazingira wa mji wetu. Kipindi cha nyuma wakati sheria na taratibu hizi zilipowekwa na mji huu watu waliozoea kuchafua mazingira waliona kawa wanaonewa na jambo hili kwao lilikuwa halitekelezeki. Lakini kwa usimamizi mzuri wa mamala za mji huu na elimu wanayoitoa kwa umma juu ya uchafu na uchafuzi wa mazingira kwa kupitia vyombo vya habari kama magazeti, redio, vipeperushi, mabango, n.k. mtizamo wa wakazi wa mji huu ulibadilika na kuendelea kuufanya mji huu kuwa miongoni mwa miji misafi duniani. Hata wageni wanaofika hapa Moshi hujihisi tofauti kwani wenyeji huwakumbushia juu ya sheria, taratibu na kanuni za utunzaji wa mazingira ili kuepuka kabisa uchafu na uchafuzi wa mazingira. Moshi ni mfano biora wa kuigwa katika miji iliyopo Tanzania kwani inatekeleza kwa vitendo sheria na taratibu za utunzaji wa mazingira ambazo zimewekwa na dunia, taifa na mji wa Moshi. Utamaduni huu tuliouanzisha wanamoshi ni laazima uenziwe na udumishwe kwa wengine kujifunza kutoka kwetu Napenda kusema kuwa, utekelezaji wa agizo la mheshimiwa raisi wetu kuhusu usafi na hifadhi ya mazigira alilotoa mara baada ya uchaguzi mwaka 2005, kwetu hapa Moshi limetekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha. Masikitiko yangu makubwa ni kwa miji mingine ambayo bado inazidi kusuasua juu ya jmbo hili. Sipendi kuitaja miji hii ila sisi wote twaijua maana kila siku kwenye vyombo vya habari tunaona na tunasikia. Mnaju hapa kwetu jiji linaloongoza kwa uchafu na uchafuzi wa mazingira ni lipi hata limewekwa kwenye orodha ya majiji machafu duniani. Ni aibu kwa taifa letu, maana miji na majiji yetu ni nyuso zetu na kama usoni utakuwa mchafu kiasi hicho, je sehemu zilizojificha itakuwaje!Ni wajibu wetu kutekeleza tamko la kimataifa, kitaifa na la raisi wetu juu ya utunzaji wa mazingira yetu. Kero ya Uchafu na Uchafuzi wa mazingira ina uhusiano wa moja kwa moja na kuendelea kuwa maskini. Mazingira machafu hayawezi kumvutia mwekezaji ambaye angeleta maendeleo kwa taifa letu. Ni wajibu wa kwetu kuendelea kuyatunza mazingira yetu ili tuvuutie wawekezaji na watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea miji yetu. Miji yetu ikiwa michafu, wageni wataogopa kuja kwani watakuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa.Tuwe wasafi jamani, Michael Mpombo, Moshi, Michael Mpombo, Moshi. 05/05/2010
    Je sisi Wafanayakazi wa ASIZE (NGOs) za Kitaifa na Kimataifa tunahitaji kuwa na umoja wetu wa Wafanyakazi ? Au shirikisho letu la Wafanayakazi ? Rejea Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu. Hermengild Mayunga 02/05/2010
    Mfumo huu utasiadia kwa kiasi fulani, Lakini ipo haja kubwa kwa Sera ya Taifa inayohusu NGO kuangalia nafasi ya Budget ya Taifa kusaidia kazi za NGO, kwa sababu kama Serikali inayouwezo wa Kutoa Ruzuku kwa Vyama vya Kisiasa bado wanayo nafasi kwa kusadia kujenga Uwezo na kusaidia Ruzuku kwa NGOs Ambazo zinafanya kazi zile za kutekeleza mipango ya Maendeleo ya Taifa. Pia uwepo utaratibu wa Sera amabao utazilazimu Aasai za Nje zifanye kazi na Asasi za Kiraia za Ndani, badala ya kuwa sasa wanakuja wanataka pia Watumishi katika Ofisi zao watoke pia huko nje. Nadhani ipo haja sana ya Kuangalia kwa Upana Sera ya Taifa kwa NGO za Kitaifa Hermengild Mayunga 02/05/2010
    I totally agree with you Noel, there are times I wonder what actually are CSOs for if they can't represent the poor people properly. In many cases they are just money making schemes. James 30/04/2010
    Collectve responsibilities, good and strict leadership (like that of Kagame in Rwanda....sio blah....blah) with well defined clear goals will take us steps forward. Africans we have a lot to learn from Rwanda and not trips to Europe and US Kelvin 29/04/2010
    Cha muhimu nikionacho mimi......Asasi za kiraia zina nafasi yake kubwa katika kupunguza umaskini uliokithiri katika jamii yetu, lakini kwa hali ilivyo baadhi zimeanzishwa kwa manufaa binafsi zaidi ya malengo yalioko makaratasini. Pendekezo langu ni kwamba kuzidishwe mfumo ambao utafuatilia na kuthibitisha ruzuku na misaada itolewayo kupitia Asasi hizo inatumika ipasavyo kwa malengo husika. Ruzuku zitolewe na ufuatiliaji uwepo kupima kama uwezeshji uliofwanywa una-impact au la......then justification kuendelea kuruzuku pale panapoonekana kuna matatizo baada ya mafanikio kuonekana kutokana na ruzuku ya kwanza ndipo ufanyike! Kelvin 29/04/2010
    Featured Topic: |
    NINI KINAFUATA ZANZIBAR?
    Useful Links
  • National civil society networks and organizations
  • Regional and global civil society networks
  • Others
  • CSO Directory
  • cso websites funded
    by fcs
  • paralegal
  • Christian Council Of Tanzania
  • Guluka Kwalala
  • Agenda Participation 2000
  • About Us | contact us | Press Room | Vacancies | Privacy Policy | Terms and Conditions | Join our mailing list | Webmail
    © 2009 The Foundation for Civil Society. All Rights Reserved.